Mapishi – Kababu (Meat Ball)

meatballs

Nawasalimu katika jina la Yesu, natumaini wote mu wazima na Bwana anaendelea kuwapigania. Leo tuangalie mapishi ya meat ball(kababu) za nyama ya ng’ombe. Ni kitafunwa kizuri sana kwa asubuhi au hata jioni.

Mahitaji

 • Nyama ya kusaga 1/2kg
 • Yai 1
 • Kitunguu maji 1
 • Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1
 • Pilipili manga kijiko cha chai
 • Chenga za mkata (bread crumbs)  kikombe cha chai
 • Kotmir majani 3
 • Chumvi kiasi
 • Mafuta ya kupikia

Matayarisho

1. Katakata vitunguu maji vipande vidogo vidogo, kisha changanya nyama ya kusaga, vitunguu maji ,kotmiri iliyokatwakatwa, vitunguu saum (tangawizi ukipenda), na chenga za mkate.(Ukitumia chenga za mkate halisi ni nzuri zaidi kuliko zile spesho za madukani). Weka chumvi na pilipili manga. Waweza pia weka pilipili mbuzi kama utapendelea.

2. Pigapiga yai na kisha uchanganye kwenye mchanganyiko wako, hakikisha vimechanganyika kabisa. Kisha tengeneza madoge madogo ya mviringo na weka pembeni. Hakikisha madonge sio makubwa sana ili nyama iweze iva vizuri.

3. Weka kikaango jikoni na mafuta na kiasi ili madonge yako yasizame, weka kababu zako kwenye mafuta na ziache ziive upande mmoja kisha geuza na upande mwingine. Zingatia moto uwe wa kiasi ili zisibabuke bali ziive hadi ndani kabisa.

4. Epua na weka kwenye sinia yenye karatasi za jikoni ili zichuje mafuta yote kisha weka mezani tayari kwa kula.

Waweza kula na chai, juis, soda au hata mchuzi wa maharage, mboga za majani n.k jinsi upendavyo mwenyewe.

Enjoy!

Advertisements

13 thoughts on “Mapishi – Kababu (Meat Ball)

 1. kwani hizo chenga za mkate nazipata wapi?naukatakata mkate au zauzwa mahali. please jibu nataka nipike this weekend.naomba uniwekee na kachori mpendwa.thanks in advance

 2. Kuna ambazo zinauzwa kwenye supermarkets ila mimi huwa natumia za mkate fresh. Nunua mkate mlaini na uchambue upate chenga ndogondogo, usiweke ile ngozi ya pembeni.
  Karibu sana, ombi lako nitalifanyia kazi.

 3. nimependa maelezo yako lakini ningependa kufaham juu ya upishi huu ambapo wengine huchanganya nyama pamoja na mkate ulioroekwa kwa kuukamua maji yote na kuuchanganya na nyama

 4. Karibu
  Unajua mapishi ni sanaa na kila mmoja anajaribu kuweka ubunifu ili kuleta sanaa bora. Wengine badaya ya chenga za mikate ndio wanatumia mkate uliolowekwa na wengine wana toast mkate kisha wanautwanga na kutumia, yote ni sawa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s