Bajia za Dengu

Bajia Dengu

Shalom,

Kuna msomaji ameomba mapishi ya bajia hivyo leo tutaangalia mapishi ya bajia za dengu.

Mahitaji

 • Unga wa dengu kikombe kimoja
 • Vitunguu maji 2 (Katakata vipande vidogo vidogo)
 • Vitunguu saumu vilivyo sagwa kijiko cha chai 1
 • Baking Powder  kijiko cha chai 1
 • Maji Kiasi
 • Chumvi
 • Mafuta ya kukaangia
 • Pilipili , Kotmiri ukipenda

Matayarisho

1. Kwenye bakuli kubwa changanya unga wa dengu na vitunguu maji na vikisha changanyika weka vitunguu saumu, kotmiri iliyokatwa katwa na baking powder. Weka chumvi kiasi kidogo.

2. Weka maji kidogo kidogo hadi mchanganyiko wako uwe mzito kisha uache kwa muda.

3. Bandika kikaango jikoni na weka mafuta, yakishachemka chota mchanganyiko wako kwa kijiko na kuweka kwenye mafuta. Angalia usiweke mara nyingi sana ili bagia zisijeshikana.

4. Zikiiva na kuanza kubadilika rangi epua na uweke mahali zitoke mafuta. Hakikisha moto sio mkali sana ili ziive na sio kubabuka.

5. Andaa tayari kwa kula na kinywaji chochote.

Enjoy!

Advertisements

10 thoughts on “Bajia za Dengu

 1. asante sana Women Of Christ.. nimefurahi kupata recipe inayohusu bagia.. Mungu awabariki sana. nitajaribu kupika wikend..

 2. Asanteni sana wamama wa Yesu.Nilikuwa napika mara hiyohiyo baada ya kuchanganya mahitaji yote, bila kuziacha ziumuke, zikawazinatoka ngumu haifai, sasa nimeweza. Mbarikiwe

 3. mie naitwa Aisha napenda sana mapishi naomba mnielekeze jinsi ya kupika vishet ntafurahi sana

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s