Mbinu za Jikoni

1. Kuondoa unga wa ngano uliogandia kwenye mikono kwa haraka.

Chukua unga wa mahindi na usugue mikono kisha uioshe na maji, unga wa ngano uliogandia utaondika kwa urahisi kuliko kuosha na maji pekee. Mbinu hii ni mahususi hasa pale unapopata simu ya haraka au inapotokea dharura na mikono yote imejaa unga unaoukanda.

2. Kugundua kama magadi (baking soda) bado yanafaa au la

Inawezekana unayo magadi kwa muda mrefu na huna uhakika kama bado yana nguvu. Chukua vinega na weka kwenye kikombe, nusu kikombe, kisha  weka kijiko cha chai kimoja cha magadi kwenye hiyo vinega, ikitoa gesi kama soda basi ujue magadi yako bado yana nguvu.

3. Kuyeyusha asali iliyogandia kwenye chupa

Chukua chupa yako ya asali (isiwe chupa ya kupasuka) na uiweke kwenye sufuria yenye maji ya moto kwa muda utaona asali yako ikiyeyuka na kutoka kwa urahisi.

4. Unapotengeneza cup cake chache kuliko uwezo wa chombo chako cha kuoka

Kama unatengeneza cup cake 10 na chombo chako cha kuokea kinachukua cup cake 12, weka maji kwenye hizo nafasi 2 zinazobaki ili kuzuia kuungua kwa chombo chako cha kuokea.

5. Kutenganisha kiini cha yai na ute

Kama huwezi kupasua kidogo na kutenganisha, njia rahisi ni kutumia funnel yenye mrija mwembamba ambao hauwezi kupitisha kiini cha yai.

6. Kutafuta vipande vya glass vilivyovunjikia kwenye maji ya mapovu kwenye sinki ukiwa unaosha vyombo

Hii sijawahi kuitumia ila nasikia inafanya kazi, chukua bakuli pana la kioo (kama glass) na uweke juu ya maji na uitumie kama lensi kuangalia vipande vya glass vilivyo ndani ya maji.

Advertisements

2 thoughts on “Mbinu za Jikoni

  1. Ubarikiwe MTUMISHI wa mungu kwa mbinu hizi za jikoni.Ushauri wangu ktk keyeyusha asali iliyoganda kwa maji ya moto, kutumia dakika zisizozidi5 kuepusha uharibifu wa asali kwa kuwaua microorganism (normal flora). pia moto kwenye asali unatabia ya kupoteza balance kati ya glucose na fructose.

    ASANTE.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s