Mipangilio ya Wiki

Maisha ya mwanamke wa miaka ya sasa yamezungukwa na mambo mengi na bila kuwa makini ni rahisi sana kuchukuliwa na masumbufu ya dunia na kumsahau Mungu na hata wakati mwingine kushindwa kuzihudumia familia zetu. Wengi wetu tu wafanyakazi wa kuondoka nyumbani asubuhi na kurudi jioni au wakati mwingine usiku kabisa, hivyo muda wa kuwa na familia ni mdogo sana.

Ili uweze kupata muda wa kufanya mambo yote yanayokuhusu bila kuegemea upande mmoja,  ni vyema ukawa na utaratibu wa kuipangilia wiki  yako kabla hujaianza. Tenga muda kila siku ya jumamosi au jumapili uwe na wakati wa kukaa peke yako bila kusumbuliwa na uipangilie wiki yako inayokuja itakuwaje. Hakikisha kila unchokitazamia kukifanya umekiweka kwenye mipango yako na pia uache nafasi kwa dharura yoyote itkayojitokeza.

Panga kuhusu kazi, maombi, manunuzi mbalimbali, mialiko uliyonayo na unayotaka kuitoa, mapishi, usafi wa nyumba, kukaa na familia, shughuli za kanisani, shughuli za kijamii, saluni, n.k. Usipende kuishi kwa kukurupuka, kuweka mipango kutakupunguzia stress na pia utapata muda wa kutosha kupumzika. Pia usipende kununua vitu ambavyo hujavipangilia na hakikisha unapata muda wa kutosha kuwa na watoto wako kila wiki.

Pangilia maisha yako na ishi kufuatana na mipangilio uliyojiwekea.

Ubarikiwe na Bwana Yesu!

Advertisements

3 thoughts on “Mipangilio ya Wiki

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s