Tunahitajika kuongea maneno ya kutia moyo na kuwajenga watoto wetu nyakati zote. Sisi tuna nafasi kubwa sana katika maisha ya watoto wetu hivyo jinsi tunavyoongea nao ni muhimu sana, katika umri wowote walionao.
Tunahitajika pia kuwaonyesha upendo kwa vitendo kama kukumbatia, kushika mkono n.k. Tusipofanya hivyo sisi, basi watautafuta mahali pengine.
Tuwatamkie watoto wetu baraka za biblia katika maisha yao, na ya watoto wao.
Tunapaswa kutawala hisia zetu hasa za hasira pale wanapotukosea au kufanya kinyume na matarajio yetu.
Hujachelewa, kama bado haujaanza kufanya hayo yote, usisite, anza sasa.
Ubarikiwe.
Advertisements
Emen. Kila siku tumuombe Mungu atuwezeshe kutembea ktk tunda la Roho! Kwa wale wenye ndoa pia tumuombe Mungu atusaidie kuwa na ndoa ambazo watoto wetu watazitamani wakiwa wakubwa. Yupo rafiki yangu mmoja aliyewahi kuniambia anatamani ndoa ya wazazi wake! Ni baraka iliyoje kuwa mfano wa kuigwa kwa watoto wetu na hata jamii kwa ujumla.