Changamoto za Wamama wa Sasa

Shalom
Kwakweli wamama wa sasa  tunachangamoto nyingi sana ikiwemo wadada wa kazi. Sikuhizi wamekuwa adimu sana, ukimpata ukikaa naye kidogo tu akishaujua mji anakuwa na kiburi au mvivu na wakati mwingine watu wanamdanganya watamlipa hela nyingi anaondoka kwa mbwembwe na baadaye anarudi analia.

Jamani wenzangu mnaitatuaje changamoto hii hasa kwa wale wenye watoto wadogo? Je kuweka wadada wawili ni suluhisho?

Advertisements

8 thoughts on “Changamoto za Wamama wa Sasa

 1. kwa kweli mimi sina mtoto ila ninaona ndugu zangu wanavyolea watoto na pia nimekaa kwa muda mfupi ughaibuni kwa dada zangu na nimeona wanavyoweza kulea watoto bila house gals. Dunia tunayoenda housegals now days sio wamekuwa adimu tu ila pia wamekuwa washirikina baadhi yao ni jambo lakusikitisha sana sababu wanakuja zaidi kwenye nyumba za wapendwa kwa nia ya kuwaharibu watoto wetu na ndoa pia kuzivunja.

  Ushauri wangu now days kuna day care centres hasa kwa wakazi wa Dar-es-salaam. Nadhani inabidi wamama wa sasa tujifunze kufanya kazi za majumbani mwetu wenyewe na pia waume zetu wajifunze kutusaidia kazi ili usije ukajikuta unachoka sana. Marekani mtu ana watoto wawili wote wadogo(CHINI YA MIAKA MITATU) na anafanya kazi masaa 8. wala hana house gal na ana nyumba ya gorofa ya kufanyia usafi; ila nilichogundua kwao waume zao ni supportive sana kwenye kufanya usafi kupika na hata kulea watoto. sio kama wanaume wengi wakitanzania ambao bado anatoka kazini anapitia vikao vya friends ambavyo havina hata faida saa nyingine. Huwa yeye na mumewe wanaamka saa 11 asubuhi na mmoja anaanza kuwaandaa kuwaogesha watoto na kupanga nguo za kuwapeleka nazo watoto day care for that day, wakati baba yao anaandaa chai ya kwao na chakula cha watoto watakachokwenda nacho day care kwa siku hiyo ladba na kufanya usafi. Mimi binafsi nilishangaa sana kuona wanavyoshirikiana na nikajifunza kuwa mahausigeli wa huku kwetu wanafanya wamama kwanza wengi kuwa wavivu na pia wanafanya wanaume kujitoa kabisa kwenye malezi wanabaki kuangalia tu TV na kusubiri chakula.

  Ushauri wangu mwingine wamama wachaMungu tunaweza kufungua day care centre yetu tuna wamama makanisani ambao ni watu wazima hawana kazi tunawaajiri then asubuhi tunapeleka watoto wetu day care ambayo ni ya wacha Mungu.

  Mwisho kwa kweli tuwe makini sana na hawa mahausigeli pia ukipata house gal mpime pia coz wengine bila kujua wanakuwa wameathirika na kwa sababu tu ya upendo wao kwa mtoto unakuta wanamuambukiza bila wao hata kujua.Kumalizia Mungu awalinde watoto wetu jamani kwa JINA LA YESU.

 2. kiukweli wadada wa kazi nadhan suluhisho ni kuwaweka kwenye maombi! linaonekana ni jambo dogo lkn kiukweli linaumiza akili moyo na hata maisha ya watoto wetu wadogo… tumwombe mungu atupe watu wa kutusaidia kazi na pia tuwaheshim na kuwanyenyekea sana maana wana nafasi nkubwa ktk maendeleo yetu kifamilia!

 3. Kwa kweli dada jackline umeongea mambo ya msingi sana, yanatugusa hasa tulio na watoto. Kwa hali ya huku nchini kupata daycare nzuri kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja na ngumu sana na baadhi yetu ni ‘single mothers’ hivyo ni lazima kwenda kazini ili kuweza kuwahudumia watoto.

  Kwa wanaoweza na wenye waume wanaofanya kazi ni bora kupumzika hadi mtoto amefikia umri wa kumpeleka chekechea ili uweze kushiriki kwenye malezi kikamilifu.

  Maombi ni muhimu sana maana nimeshuhudia wadada wenye mapepo na waliotumwa kuangamiza watoto. Kwakweli hii ni changamoto kubwa, wadada wengine mtoto akiwa anasumbua kula wala haangaiki naye, anampa maji tu mchana kutwa. Tunamwitaji Mungu sana katika hili.

 4. Kwa upande wangu naona wamama tujifunze kumiliki nyumba zetu ili ma-house girl watuheshimu.Wengi wana upeo mdogo wa maisha.Mchukulie house girl kama mdogo wako so ajijue kuna siku ataondoka akaanzishe maisha yake na ajue treatment yako hiyo ni kwa sababu ya Ubinadamu wako asije akakuzoelea akajua hapo ndio amefika.Kinachotutesa wengi ni kuwa tunawanyenyekea kiasi kwamba wanapata ile feeling kwamba sie bila wao tumekwisha na hii ni kwa sababu ya upeo wao mdogo.Housegirl lazima akukute we’ mwenyewe uko smart (kwa kazi zako za nyumbani) kiasi kwamba aogope ajue mama mwenye nyumba mwenyewe anazijua kazi vizuri (Yaani uwe kiongozi mzuri wa kazi zako za nyumbani).Hapo mtaheshimiana,lakini akikukuta mwenzangu na mie ndio uko sebuleni unataka funguo iko kwa coffee table mpaka umuite dada! hapo lazima akupande kichwani.Yaani muonyeshe kuwa we’ me nimekuweka ni kwa sababu nafanya kazi zinazokula muda wangu other wise we’ ni msaidizi tu na sio mfanyikazi wa kazi zangu za ndani.Tatizo wengi wetu tunakuwaga na ile feeling ya dharau kwamba wao wana shida na sie ndo wenye hela so we can treat them vyovyote vile.Me nadhani handling ya nyumba yako kwa mifano itamfanya akuheshimu,by the way for those of us ‘married’ waume zetu walituchagua because they proved we’re hard workers.So let’s be confident mamas with our homes because we’ve been entrusted to start them be it single/married bila kusahau UPENDO + MAOMBI kwa nyumba zetu.

 5. Shalom, pia kina mama tusisahau kuwapekua wafanyakazi kwenye mabegi yao wanayokuja nayo. Nina wifi yangu yeye alipata msichana wa kazi kumbe ndani ya begi lake kaja na madawa kibao na alikuwa anawakorogea kwenye chakula. Sijui alikuwa ana lengo gani haswa na hii familia, hivyo cha msingi tuwapende lakini tusiwaamini tukajisahau. Wale wanakuja na malengo yako, kuna wengine ndio wana shida na wanataka kufanya kazi wapate kipato cha kujikimu lakini wengine ni tofauti kabisa, na hawa ambao wanasema wameokoka ndio haswa tuweni macho nao. Nilishapata kama wawili maana na mimi ni mpendwa nikaona nichukue waliookoka lakini kuna ambao wamebeba roho za kusambaratisha familia tuwe sana macho nao na ni wazuri sana kwa kufungua maombi na kuimba mapambio. Ukimpata wa hivyo mtafutie kikundi cha waombaji halafu muombe pamoja kama kweli ni wa Mungu itajidhihirisha lakini kama kaja kama agent basi pia ile nguvu ya Mungu itaweka kila kitu wazi.

 6. Bwana Yesu asifiwe sana!

  Kwa kweli mimi pia nimepitia shda hii, nina watoto wawili tena wanaofuatana sana. Miaka 3, na miwili kasoro. Katika mabinti niliowah kuwapata, moja alikaa miezi 1, 3, 1, 9 na 6. Kipindi chote hiki nilikuwa nakaa na mmoja ila ilifika wakati nikawa busy sana na kazi pia majukumu yakaongezeka, watoto wawili, na kazi za nyumbani. Nikaamua kuwa na wawili.

  Ushauri wangu ni kwamba wasichana wawili ni muhimu pale ukiwa na majukumu mengi na haswa watoto wakishakuwa wawili chini ya miaka 5. Kwa kweli kazi zinapokuwa nyingi sana wasichana huwa wanaondoka. Pia, tusiwaminyie sana mshahara, kazi wanazofanya kwa kweli ni nyingi.

  Ushauri mwingine ni pale unapoamua kuajiri wawili, hakikisha hawatoki sehemu moja. Watashawishiana na siku wakiondoka huwa wanaondoka kwa pamoja!

  Ubarikiwe na Bwana.

 7. Margaret umeongea mpendwa.Nimempata dada wa kazi sijamlipa hata mshahara wa kwanza amejitambulisha yeye ni mlokole.Mungu kanikataza kumkubali kwa maneno yake.Kwenye kuabudu kasema hawezi kuabudu kanisa lingine zaidi ya la kipentekoste.Juzi nilipata wageni ambao ni wa rika langu,nikamwambia aandae vinywaji.Kwa kufurahia kuonana tukataka kujisahau tusiombee vinywaji kabla ya kunywa (kawaida huwa naombea vinywaji kabla wageni hawajatumia),kabla hatujaanza kunywa Roho Mtakatifu akaninong’oneza mwambie dada aombee vinywaji.Ilikuwa utafikiri kamwagiwa maji ya baridi!Kwa kweli akaishia tu kuchekacheka kisha huyo akaondoka eti sikujiandaa.Yaani kwa shuhuda zake na maneno yake sikutegemea kama kuombea vinywaji lingekuwa swala la kujiandaa!Wangekuwa watu wazima sana ningesema labda aliogopa ila mwe!

 8. BWANA YESU ASIFIWE ”’kwa kweli wadada wa kazi ni shida ,mimi mdada wangu nilikuwa namnyenyekea na kumjali mpaka Mr akawa ananifokea baada ya muda akaanza urafiki na majirani anashinda huko mpaka usiku,muda mwingine anatoka bila kuaga nilijaribu kukaa nae kumueleza jinsi dunia ilivyo akanisikia na akabadilika.Siku hiyo akaniibukia na kuniambia dada yake anataka kumsomesha hivyo anatakiwa kuondoka.
  Baada ya muda mdada aliondoka nikafanya uchunguzi nikagundua yuko dar anafanya kazi kwingine na mshahara ni mdogo kuliko niliokuwa namlipa huku na mimi nilimpa ahadi ya kumsomesha,swali nililojiuliza alikosa nini kwangu?mpaka sasa sina mdada imenibidi nikiwa naenda kazini nimuache kwa ndugu zangu ingawa ni ngumu kwa sababu mara nyingi unajikuta unachelewa kazini.
  Nilichojifunza wadada huwa hawana msimamo na malengo ktk maisha huvyo vitu viwili wangekuwa navyo wasingeyumbishwa na mtu hasa majirani na pia malengo yangewawekea uwezo wa kujua muda husika wa kufanya kazi ili kutimiza malengo yao.
  .

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s