Ratiba ya Chakula – Updated!

Shalom

Wengi wenu mlikuwa mnaomba niwatumie ratiba ya chakula iliyopangiliwa tayari, hii hapa na unaweza kuongezea vyakula vingine ambavyo unadhani nimevisahau nawe huwa unavitumia.

Ubarikiwe.

RATIBA YA CHAKULA KWA WIKI updated

Advertisements

19 thoughts on “Ratiba ya Chakula – Updated!

 1. Unaweza pia ukaongeza vitafunwa mbalimbali kwa ajili ya kuchangamsha breakfast mf:maandazi,bajia,doughnuts,half cakes,kalimati,skonzi etc au hata kababu,egg-chops na sambusa ukaviweka kwenye friji angalau vikasogeza week.Kama una nafasi week end ni muda mzuri kuviandaa kwa kiasi,sema umeme wetu.Firigisi roast ni nzuri pia hapo kwenye breakfast ya Jumamosi.Supu/mchemsho pia hufaa kwa Jumamosi kwani tuna muda mwingi nyumbani.Kwa wale wapenzi wa uji wa lishe si vibaya ukiwepo breakfast ya kila siku.

  Juice na fruit works ni vizuri pia kuzingatiwa.Ikiwezekana tufundishane hapa bloguni namna ya kuandaa aina mbalimbali za fruit salad na juice mbalimbali kwa kadri ya matunda yanayopatikana kwenye jamii yetu.Fruits/Juice ni vizuri vikawepo kila mlo.

  Vichangamsha meno mf:karanga(kuna za mayai),korosho,visheti/vivunja meno,keki(ile ya birthday kabisa decoration sio lazima),biscuits,ufuta,vipande vya kuku vilivyokaushwa,vidole vya samaki(fish fillets),kaukau etc ni vizuri haswa kwa mida ile kati ya lunch na dinner plus juice/maziwa/chai/kahawa huchangamsha sana kiasi kwamba ukajikuta hata jioni huna haja ya kupika heavy dinners.

  Milo ya jioni unaweza ukadesign vifuatavyo pia:

  1.Chips/Ndizi za kukaanga+nyama ya kukaanga(ng’ombe,kuku,samaki)+tambi bila kusahau kachumbari(au roast lolote) watu wasije wakakabwa!

  2.Chapati za kumimina+maini roast+tambi/macaroni.

  3.Magimbi/Mihogo vyenye nazi/Viazi vitamu vya kuchemshwa tu au kusongwa+maharage+samaki wa kukaanga (mie hupendelea vibua kwa huku Dar)+vegetables.

  4.Ijumaa since weekend inaanza jioni unaweza ukaanda roast la kuku/ng’ombe(au soup zake)+chapati za kusukuma.Naipenda hii kwa sababu zile chapati unaweza ukapika mpaka za soup Jumamosi asubuhi ikawa aubuhi una kazi ya kupasha tu.

  *Veggies ni muhimu kwa kila milo ya mchana na usiku.
  *Tusisahau kuwa na appertizers mf:pilipili ya kupika ukaiweka kwenye friji,mango pickle,mbilimbi pickle etc.
  *Tusisahau kuyaleta nyumbani yale tunayoyaona sehemu tutembeleazo mf:migahawani,mashereheni,mahotelini,kwa marafiki,mitandaoni ili mradi tu familia zetu zisiyaonee kwa watu tu.Hii ni pamoja na mpangilio mzuri wa meza unapotenga chakula chako,good table arrangement inabariki kwa kweli hata kama mlo wako sio draft ila ni mdako tu!

  Ni hayo tu kwa leo.

 2. Asante sana kwa ratiba ya chakula,imepangika vizuri sana.Kupitia hii naweza kurekebisha ya kwangu.Mungu akubariki.

 3. Nimefurahia sana maelezo yako dada Cathy, ni muhimu sana wamama kuwa wabunifu linapokuja suala la chakula majumbani mwetu. Unaweza ukawa na ratiba ya kawaida kwa ajili ya dada siku za kazi na weekend unaingia mwenyewe jikoni na kuwapikia vyakula vizuri na kwa ustadi. Jumamosi unaweza andaa supu kama kifungua kunywa kwa familia nzima.

  Nitaweka hapa jinsi ya kuandaa juisi na saladi mbalimbali. Ubarikiwe sana

 4. dada women of christ. ratiba yako ni nzuri sana na umejitahidi kuangalia watu wenye uwezo wa chini na kati ila wewe dada cathy umeangalia zaidi watu wenye maisha ya juu.tengeneza basi na ya watu wa maisha ya chini na kati.

 5. Tunashkuru sana kwa ratiba ni nzuri na tumeipenda, ila pia tunaomba ratiba ya wale wafanya diet maana hii inaweza kunenepesha fasta, kwa sie tunaofanya diet tafadhali,

 6. nashukuru kwa ratiba nzuru …itanisaidia saaaana.ila naomba kuelekezwa kupika chapati za kumimina vizuri

 7. Mrs.N yaani me mwenyewe nilikuwa nayaonea maisha hayo kwa watu ambao nawaona wanazo kiukweli ni rahisi mno unakuta hela ni ile ile ya kukidhi ratiba zetu za kikawaida ya ugali mchana na wali usiku na kwa maisha ya wengi wetu mchana hatushindi majumbani so unakuta muda ambao mara nyingi tuko wote(sehemu kubwa ya familia) ni jioni so ukakuta ile gharama ya mchana ikakidhi almost yote kwa usiku.Lakini otherwise ni vizuri pia tukajua kuwa tunastahili vizuri me kuvioneaga mahotelini roho inaniuma kweli.Mimi nilikuta watu wa familia yangu kumbe hawapendi heavy dinners like ugali/wali tu kila siku usiku nilipo-test light dinners they were like wow! Siku nyingine tunakunywa breakfast usiku to bed we go au glass za juice na hizo bites ambazo unakuwa unaandaa basi we call it a night sanasana labda weekend ndiyo unajikuta una kazi ya kupika sana mchana kwani watu karibia waote wanashinda nyumbani.Ni hayo tu.

 8. God bless you,nimehangaika sana kujua nipange vipi ratiba hapa nimepata suluhisho…Thank you so much

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s