Maombi na Maombezi

Shalom

Wapendwa tuendelee kuleta mahitaji yetu hapa ambayo tutakuwa kwa pamoja tunashirikiana kuyaombea kwa wikiend yote. Mungu wetu ni mwaminifu na tukipatana kwa umoja kumwita juu ya jambo fulani hakika atalitenda kwa utukufu wa jina lake.

Weekend hii kwa pamoja tuombee wasichana ambao wanakata tamaa kwa sababu ya kuona kuwa wanachelewa kuolewa. Tuwaombee Mungu awape hekima na burasa ya kiMungu katika kuwatambua wenza wa kutoka kwa Mungu, wapewe uvumilivu wakimngoja Bwana ili wasije fanya uamuzi utakaowaletea majuto.

Kama una hitaji lolote unaweza liongezea hapa ili tuombe kwa pamoja.

1Yohana 5:14-15 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomuomba.

Advertisements

4 thoughts on “Maombi na Maombezi

  1. Sina haja ya kuongeza ila naona hilo ombi ni jema sana na mimi ntahusika kuliombea.

    Barikiwa

  2. Mmefany lililo jema;mim ninaomba tuwaombee vijan waliooa ndoa zinavunjika sana;namim inanihusu

  3. nami pia nahusika mungu anisaidie kumjua yupi ni mume mwema kwangu nimekuwa naa wakati mgumu sana ,na ninaomba hayo maono yatoke kwake shetani asipate nafasi ya kutoa maono yake.ubarikiwe

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s