Bwana Uliyewaita

Wimbo huu umekuwa ndani yangu kwa muda mrefu sana:

1. Bwana uliyewaita watakatifu wako,
wawe mitume wachunga wachunge kundi lako.
Wanyonge na wenye hofu, wakawa mashujaa
Na wapole wa kunena, wasiwe kunyamaa.

2. Hata leo wawataka watakatifu wako,
Nawe wauliza tena ni nani aliyeko,
Atakaye nimtume afundishe vijana,
Nitayari Bwana wangu nitume mimi Bwana.

3. Nitume na mimi Bwana kama ulivyotumwa,
Habari za msamaha na dhambi kutubiwa,
Niwahubiri wakosa na waliopotea
Wokovu u kwake Bwana aliyewafilia.

3. Astahiliye hapana kutamka habari,
Lakini wewe waweza kutufanya tayari,
Neno lako tulijue tupe na Roho wako,
Hayatakuwa ya bure haya maneno yako.

Tuimbe pamoja tukimaanisha!
Ubarikiwe.

Advertisements

11 thoughts on “Bwana Uliyewaita

  1. yes dada,huu wimbo una maana kubwa sana katika kutukumbusha wajibu wetu in serving God as we live..asante dada

  2. WIMBO HUU HUNIKUMBUSHA KUWA KAZI HII NIIFANYAYO HAITAKUWA YA BURE. UBARIKIWE MPENDWA

  3. Mm wimbo naukubali na ninajua kuuimba inabidi tuandae siku maalum tuiite BWANA ULIYEWAITA na tukutanishe makundi yaimbe wimbo huu utafurahii.Na aliyeutunga mnamjua kwa nn aliutunga njoni nitaweleza

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s