Je Upo na Yesu au Umempoteza?

Shalom

Luka 2:42-46 Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu; na walipokwisha kuzitimiza siku, wakati wa kurudi kwao, yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake walikuwa hawana habari. Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika Hamas zao na senza; na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.”

Wazazi wa Yesu baada ya kumaliza ibada Yerusalemu walianza safari ya kurudi nyumbani na walidhani Yesu yupo pamoja nao, hawakuhakikisha hilo bali waliendelea na safari wakiwa na dhana hiyo. Baada ya mwendo wa kutwa ndipo walipotambua kuwa hawapo naye, cha ajabu badala ya kurudi walikotoka wao wakaanza kumtafuta katika jamaa zao na wenzao walipomkosa ndiposa wakakumbuka kurudi Yerusalemu. Iliwachukua siku tatu kumpata baada ya kumpoteza kwa kutwa moja.

Katika maisha ya sasa yaliyojaa shughuli na masumbufu mengi ni rahisi sana kumpoteza Yesu na kudhani kuwa upo naye. Watu wengi wameshampoteza Yesu ila hawajagundua wanaendelea na safari wakidhani yupo kati yao. Unapompoteza Yesu na kuja kugundua kuwa umeshampoteza inachukua muda mrefu zaidi kumpata, wazazi wa Yesu iliwachukua siku tatu baada ya kumpoteza kwa kutwa.

Jichunguze na kujihakikisha kama bado upo na Yesu na ukigundua umempoteza usizunguke zunguke wewe nenda mbele za Mungu na uombe kuurejeza upya uhusiano wako naye. Soma neno la Mungu, omba kwa bidii na kuyatenda yale aliyotuamuru. Inahitaji bidii na kujitolea kumtafuta Yesu uliyempoteza, jiangalie sana usijempoteza. Amen.

Advertisements

7 thoughts on “Je Upo na Yesu au Umempoteza?

 1. Ni muhimu kujichunguza kama bado uko na Yesu ndani yako kila siku. Yawezekana umeanza kurudi nyuma na Yesu hayupo tena ndani yako.Utajuaje kama umeanza au umempoteza? tafadhari soma mafundisho yafuatayo na itakusaidia kujitafakari mwenyewe;

  DALILI ZA KURUDI NYUMA KIROHO NI ZIPI?
  SOMO LINA MAENEO MAKUU YAFUATAYO:
  1. UTANGULIZI
  2. TAFSIRI 11 ZA KIROHO ZA KURUDI NYUMA
  3. SABABU 15 ZINAZOWAFANYA WATU KURUDI NYUMA KIROHO
  4. MADHARA YA KURUDI NYUMA KIROHO
  5. DALILI 17 ZA KURUDI NYUMA KIROHO
  6. HATUA 10 ZA KUKUSAIDIA USIRUDI NYUMA
  7. MAJUKUMU TULIYONAYO KWA WALE WALIORUDI NYUMA

  Mwanzo 19:26
  ‘’Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake akawa nguzo ya chumvi’’. Mungu alimuonya Lutu wasitazame nyuma lakini mkewe Lutu alipoyapuuza maonyo hayo na kutazama nyuma,yakampata mambo mazito.
  Sisi nasi baada ya kuokoka ni vizuri tukawa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na jambo hili kwamba kuna madhara makubwa unaporudi nyuma kiroho au kuacha wokovu.HATUKUJIOKOA,AMETUOKOA YEYE MUNGU.
  Mungu kwa upendo,huruma,neema na rehema zake ametuokoa kutoka katika utumwa mzito wa dhambi.Hakutaka twende motoni kwenye mateso makali na ndiyo maana maandiko matakatifu yanasema’’ tumeokolewa kwa neema na sehemu nyingine Yesu anasema siyo sisi tuliomchagua yeye,bali ni yeye ametuchagua sisi (soma Waefeso 2:8-9,Yohana 15:16).
  Kwa sababu hiyo,tunapaswa kukubali upendo wa Mungu kwetu,ukizingatia amekwishatuonya kwenye Neno lake kwamba hakuna mwenye dhambi atakayemwona Mungu (Ufunuo 21:8, 1 Korinto 6:9-10,Wagalatia 5: 19-21).Neno la Mungu vile vile linaitwa ‘’Mausia ya Mungu kwetu’’(Warumi 3:2).Kupuuza mausia ya Mungu kwetu ambaye ndiye Baba yetu na kuamua kurudi nyuma NI HATARI SANA.
  Sasa ili ufahamu vizuri kurudi nyuma na kuacha wokovu ni nini mbele za Mungu, hebu tuangalie tafsiri yake kiroho.

  TAFSIRI 11 ZA KIROHO ZA KURUDI NYUMA NA KUACHA WOKOVU.
  1.Ni sawa na mbwa aliyerudia matapishi yake mwenyewe na nguruwe aliyeoshwa
  na kurudi kugagaa matopeni.Biblia inasema ni mpumbavu tu ambaye atafanya upumbavu tena baada ya kuokolewa na anafananishwa na mbwa anayeyarudia matapiko yake (soma Mithali 26:11)
  Dhambi mbele za Mungu ni sawa na matapiko au matope machafu.Wakati wa kuokolewa tulisafishwa uchafu huo kwa damu ya Yesu Kristo,sasa kugeuka nyuma na kuacha wokovu ni kuyarudia matapiko hayo na kugagaa katika matope machafu.Mtu mwenye akili timamu naamini hatafanya hivi.(2 Petro 2:20-22)
  2.kugeuka na kutoka kwa Mungu (au unaachana na rafiki yako wa karibu Mungu) –soma 2 Wafalme 11:9.
  3. Unageuka na kuacha upendo wa kwanza (Ufunuo 2:4 )
  4. Unageuka na kuiacha habari njema (Wgalatia 1:6,3:1-5 )
  5. Unamgeukia shetani au unarudi kwa shetani.
  Kumbuka unapookoka unamkana shetani na kazi zake zote.Kitendo cha kurudi nyuma maana yake unaamua kurudi ulikotoka (1 Timotheo 5:15 ).

  6. Unarudi maovuni (Zaburi 125:5)
  7. Unarudi ulimwenguni.
  Mara tu unapookoka uraia wako unabadilika, unakuwa siyo raia wa ulimwengu huu tena.Kwa hiyo unaporudi nyuma unaurudia ulimwengu huu unaopita. (soma 2 Timotheo4:10)
  8. Ni kumsulubisha Mwana wa Mungu kwa mara ya pili na kumfedhehi kwa dhahiri.Kurudi nyuma na kuacha wokovu ni kumpiga misumari tena Yesu Kristo na Kumgongomea msalabani huku ukimvisha taji la miiba tena,kumpa siki anywe na kumchoma ubavuni kwa mkuki.Isitoshe unamtemea mate na kumdhihaki huku ukimwambia ‘’ jiokoe mwenyewe’’.Mtu mwenye hofu ya Mungu hatadhubutu kufanya hivi hata siku moja.(soma Waebrania 6:4-6)

  9.Ni kumsaliti Yesu.
  Yuda alimkaribia Yesu ili kumbusu.Yesu akamwambia Yuda ‘’wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu’’ (Luka 22:47-48). Kwa nini umbusu Yesu halafu umsaliti? Kumbuka jambo hili lilimgharimu Yuda mauti ya milele.Ni maombi yangu hatutamsaliti Yesu.

  10.Ni kumkana Yesu.
  Wakati wa kuokoka ulimkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako na kumkataa shetani na kazi zake zote,sasa unaporudi nyuma maana yake unamkana Yesu na kumpokea shetani na kuwa bwana wako (Mathayo 26:71-72) Petro alimkana Yesu baadaye akagundua kwamba amefanya machukizo akatubu na kusamehewa.Mungu akusaidie usimkane Yesu kwa vitu vinavyopita na kuharibika
  11.Ni kumtukana Bwana
  Namna yoyote ya kurudi nyuma na kuacha wokovu ,ujue unamtukana Bwana na
  maandiko yanasema mtu wa namna hiyo hatakosa adhabu (soma Hesabu 15:30)

  SABABU 15 ZINAZOSABABISHA WATU WENGI KURUDI NYUMA KIROHO;
  1.Kukosa viongozi wanaofundisha kweli ya Neno la Mungu
  (soma 1 Tim 6:10,Kutoka 32:1,Matendo 20:30,2 korinto 11:4,Waamuzi 2:19)
  2. Kuupenda ulimwengu huu wa sasa
  (soma 2 Tim 4:10,Mithali 24:1,Warumi 12:2)
  3.Kukataa kuonywa,kukaripiwa na kuelezwa sawa na Neno la Mungu
  (soma Mithali 15:5,9:8 )
  4.Kukaa katika ushirika uliojaa maasi (soma Mathayo 24:12)
  5.Kukosa mizizi na hivyo kuogopa dhiki na mateso
  soma Luka 8:13,Mathayo 13:20-21,1korinto 3:1-3, Waebrania 5:11-14)
  6.Mahusiano mabaya (soma Hosea 4:17)
  => Kuoa au kuolewa na mtu asiyeokoka (1 Wafalme 11:4,Nehemia 13:26,
  2 Korinto 6:14)
  => Marafiki wabaya (soma 1 Korinto 15:33,1 Petro 4:2-4
  => Kutokushirikiana na wenzako (soma Waebrania 10:25).
  => Ugomvi kuhusiana na tendo la ndoa (soma 1 Korinto 7:5)
  => Magomvi,migawanyiko,chuki,wivu,ghadhabu,masingizio nk (soma Mathayo 18:35,1 Timotheo 6:20-21,2 Korintho12:20-21)
  =>Uzinzi (soma Mithali 29:3)
  7.Kuachana na maisha ya maombi (Zefania 1:6,Luka 18:1)
  8. Kutokuamini ( zaburi 106:24)
  9.Kutaka kuwapendeza wanadamu/kutafuta utukufu kwa watu(Galatia 1:10, Yohana 5:44 )
  10. Kiburi (Mithali 16:18, yeremia 8:12, Hosea 13:6, Yohana 5:44,Luka 18:11-12,1 Korintho 10:12,1 Yohana 2:16 )

  11.Uasi wa mioyo migumu. (1 Samwel 15:11-23,Nehemia 9:17-26,Zaburi 106:43,Isaya 1:19,Yeremia 2:27-32)
  12. Usumbufu (stubborness ) soma Waamuzi 2:19,1 Samwel 12:25,Zakaria 7:11-
  13. Kujiamini kupita kiasi ( over confidence) Mathayo 26:33,Galatia 5:4,Ufunuo 3:17.
  14. Tamaa za mwili (soma Warumi7:4-5,2 Samwel 11:13,12:1-13,2 Petro 1:4,1 Petro 2:11
  15. Kunung’unika (soma kutoka 17:3)

  ADHABU AU MADHARA YANAYOMPATA MTU ALIYERUDI NYUMA
  1. Unaharibika kiroho na kukosa matunda (spiritual ineffectiveness and decay)
  Soma warumi 8:13,2 Petro 2:20-22
  =>Aliyerudi nyuma anakuwa hana ushuhuda mzuri kwa wengine (soma 2 Samwel 12:14, Mithali 28:10)
  => Unapoteza furaha (soma Zaburi 51:12,Waamuzi 2:15,10:9)
  => Huna tena hofu ya Mungu (soma Yeremia 2:19
  2. Huwezi kuhisi tena uwepo wa Mungu. (soma Hesabu 14:43,Isaya 59:2)
  3. Hukumu ya Mungu (soma Kutoka 20:5,Kutoka 34:14,Zakaria 7:12)
  4. Hujibiwi maombi (soma Isaya 59:2) na hivyo;
  => Utaonewa na maadui –Hesabu 14:43 torati28:58-61)
  => Kifo kabla ya wakati ( kumbukumbu 30:17-19
  => Madhara kwenye familia ( soma 2 Samwel 12:9-12)
  5. Kupoteza nafasi (loss of position)
  => Unapoteza ushirika na Mungu (soma 1 Yohana 1:6-7)

  KUGEUKA NYUMA HUANZIA MOYONI:
  Mtu aliyeokoka, anapogeuka nyuma jambo hili huanzia moyoni. Mtu wa namna hii anaweza akawa anaonekana katika jumuiya ya watu waliokoka na salamu yake kubwa ni ‘’Bwana Yesu asifiwe’’.Lakini Mungu anapomuangalia moyoni mwake alikwisha kurudi nyuma.Mtu huyu kwa macho ya nyama anaonekana anakwenda kanisani au mbunguni kumbe moyo wake tayari ulisharejea kwa shetani. (Soma Matendo ya Mitume 7:39)
  Kwa vile kurudi nyuma kuananzia moyoni,anayejua kwanza kabisa ni Mungu halafu mtu mwenyewe na mwisho shetani .

  DALILI ZA KURUDI NYUMA KIROHO
  1.Mtu anauacha ule upendo wa kwanza (hawamtafuti Bwana kila wakati kama
  kipaumbele chao cha kwanza); Wako busy na mambo ya dunia hii (Ufunuo 2:4)-
  nyuma maana yake unaamua kurudi ulikotoka (1 Timotheo 5:15 ).
  2.Udhuru unakuwa mwingi katika mambo ya Mungu kama vile hawajahi kufanya
  huduma.
  3.Marafiki zake ni wale walioacha kumtumikia Mungu;
  =>Mtu aliyerudi nyuma hutafuta marafiki ambao wamerudi nyuma pia.
  =>Watu hawa huunda jumuiya zao ili kutiana moyo katika taifa lao la kurudi
  nyuma.
  4.Wana uchungu na wapinzani dhidi ya mwili wa Kristo na mamlaka za kiroho (soma
  matendo ya Mitume 20:28)
  5.Maisha yao yanafanana na ulimwengu na siyo Kristo (soma Yakobo 4:4)
  6. Hawalifuatilii tena lile kusudi la Mungu juu ya maisha yao.
  7. Hawalifurahii tena Neno la Mungu
  =>Hawafurahii tena mafundisho kama mwanzo hasa mafundisho ya utakatifu na
  haki
  8. Siyo mtii tena wa Neno la Mungu
  9. Anayazoea mafundisho ya Neno la Mungu na kuyaona ya kawaida (hofu ya Neno
  la Mungu imeondoka) –isaya 66:2
  10.Hapendi kuonywa na kukaripiwa hata kama anafanya kinyume na mapenzi ya
  Mungu.
  11.Anafurahia mapambio na kwaya kuliko Neno la Mungu
  12.Anapofanya dhambi hakuna hukumu ndani ya moyo wake kama zamani
  13.Hataki kuongozwa na Neno la Mungu wala kuwatii watumishi wa Mungu.(soma
  Mithali 14:14)
  14.Kutokupenda kuonana au kukutana na watumishi wa Mungu (anawakwepa)
  15.Hamu ya kuomba ,kufunga ,kusoma Neno inapotea
  16.Kiburi. (kuona kuwa anaweza kila kitu
  => Mwanzo ulipookoka ulikuwa mnyenyekevu
  17.Ujuaji mwingi (much know)

  HATUA 10 ZA KUKUSAIDIA USIRUDI NYUMA
  1. Fanya tathmini ya maisha yako ya kiroho kila mara. (1 Korintho 13:5)
  2. ukiona kuna dalili za kurudi nyuma,rudi kwa Yesu haraka(Waebrania 3:12-13)
  3. Nenda mbele za Mungu kila siku kwa toba.
  4. Mtafute Bwana kila siku kwa moyo wako wote (1 Nyakati 28:9)
  5. Kaa katika Neno la Mungu kila siku, jifunze Neno
  6. Kaa pamoja na waamini wenzako kila mara (Waebrania 10:25)
  7. Simama imara katika imani yako,tegemea nyakati ngumu katika maisha yako ya ukristo.(Mathayo 10:22)
  8. Usiyumbishwe (1 Timotheo 4:15-17)
  9. Kimbia mbio za ushindi (run the race to win). 1 Korinto 9:24-25,1 Timotheo 4:7-8
  10. Kumbuka mwenyewe kile alichokifanya Yesu maishani mwako huko nyuma.(soma Waebrania 10:32-39
  11. Uwe na muda wa kukariri maandiko,yatakusaidia nyakati ngumu.
  12. Jizoeze kusikiliza nyimbo za kikristo ili kuifanya akili na moyo wako uwe kwa Mungu
  13. Uwe na marafiki wa kikristo/waliokoka ili uwe na mtu wa kumwita unapokuwa dhaifu.
  14. Jishughulishe na miradi au shughuli za kanisa na wapendwa wenzako.
  15. Maombi (soma Marko 14:38,Luka 22:46
  16. Uwe na bidii na mambo ya Kimungu.(soma Waebrania 6:11,2 Petro 1:5-7)
  17. Tembea katika Roho. (soma Galatia 5:16,Luka 4:1-14

  MAJUKUMU ULIYONAYO DHIDI YA WALIORUDI NYUMA.
  Kila mwamini analo jukumu au mzigo dhidi ya waliorudi nyuma;.
  1.Sisi ni watunzaji wa ndugu zetu. (soma mwanzo 4:9)
  2.Tubebane au tuchukuliane mizigo (soma Galatia 6:2)
  3.Tuonyane sisi kwa sisi (soma Hesabu 10:25)
  4.Inabidi tuombe mara kwa mara kwa ajili ya ndugu zetu (soma zaburi
  80:3,85:4,Yeremia 13:17,Luka 22:31-32
  5.Kuwarejeza kwa upya ndugu zetu kwa roho ya upole (soma Ezekiel 3:1-
  21,Hosea 8:1,Yohana 8:32,Galatia 6:1,1 Timotheo 4:6Hesabu 3:12-13)
  6.Kuna taji linawasubiri wale wote waliowarudisha kundini waliorudi nyuma
  (soma Yeremia 3:22 kwamba ’’Rudini enyi watoto waasi,mimi nitaponya
  maasi yenu,Tazama tumekuja kwako,maana wewe u Bwana Mungu wetu’’
  Barikiwa sana usomapo somo hili.

 2. Bwana yesu asifiwe. Hongera kwa kazi ya Mungu. Naomba mafunzo ya kristo kwa njia ya email. Mbarikiwe sana.

 3. Shalom.
  Mungu awabariki kwa kazi nzuri ya Mungu mnayoifanya. Somo hili limenifungua sana katika uhusiano wangu na Mungu.

 4. Bwana Yesu apewe sifa.nimefarijika sana kwa kazi nzuri ya kueneza injili kwa njia hii ya kusambaza mafundisho haya,

  Mungu awabariki sana,songeni mbele.

  Mwl Derrick

 5. NAOMBA MZIDIKUFUNDISHA MASOMO HAYA WATU WENGI WAMEACHA WOKOVU NA KUFATA YA SHETANI,HASA WATU WALIOOKOKA,WANAFAHAMU SHERIA YA MUNGU NA NENO LINASEMA NIN?ANAVUNJA AMRI ALIZOWEKA MUNGU ANAZINI YANITABIA ZA AJABU AJABU!SIELEW NI KWANIN

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s