Upweke

Upweke ni kitu kibaya na kina uzuri wake wakati huohuo.

Ni katika upweke wa kuuzwa na ndugu zake utumwani Yusufu alipita katika magumu lakini mwishowe Mungu alimtokea.

Ni katika upweke wa kuchunga peke yake porini Musa alitokewa na Mungu na kupewa jukumu kubwa la kuwakomboa Israel.

Ni katika upweke wa kuchunga porini Daudi alivamiwa na dubu na simba lakini Mungu alimshindia yote.

Ni katika upweke wa kutupwa katika tundu la simba Daniel alimwona Mungu na kutoka salama.

Ni katika upweke wa kutupwa katika kisiwa cha Patmo Yohana alitokewa na Mungu na kupewa mafunuo makubwa ya kitabu tunachokisoma leo cha Ufunuo wa Yohana.

Kwa hiyo tusiuogope upweke, katika huo kuna uzuri wake pia. Kwa kuwa mapenzi ya Mungu hayawezi kukuweka mahali ambapo neema yake haitakulinda.

Kutoka kwa Kate M.N

Advertisements

2 thoughts on “Upweke

  1. kweli,
    nipo mpweke ili kupunguza mawazo ya kumuwaza mume wangu nimegundua kumbe nina kipaji kizuri cha utunzi wa hadithi. Namshukuru Mungu na ninalifanyia kazi.. Sikujua ni kwa sababu ya upweke nilionao hadi niliposoma hii post yako. barikiwa mtumishi

  2. KWELI
    NIPO MPWEKE KWA KUACHWA NA MPENZI WANGU LAKINI NIMEJIKUTA NIMEPATA NAFASI YA KUOMBA KWA AJIRI YA FAMILIA YANGU KWA MUDA MREFU SANA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s