Kutoa Taarifa au Kuomba Ruhusa?

image

Shalom
Kuna mama mmoja mdogo wake wa kiume waliyefuatana naye alikuwa anaoa na ndoa ilikuwa inafanyika kwenye mji tofauti na anapoishi. Yeye alijua kuwa ni wajibu wake kama dada mkubwa kuhuhuria na kwa sababu mume wake alikuwa anafahamu hilo na hata amechanga hakuwa na wasiwasi kwamba ataenda. Wiki mbili kabla ya harusi akamwambia mumewe kuwa atasafiri kwenda harusini mumewe akakataa, na hakubadili msimamo. Yule mama aliumia sana ila hakuwa na jinsi akabaki, sababu mumewe alisema hawezi kuruhusu watoto kubaki peke yao, mama huyu alikuwa mama wa nyumbani.

Jambo hili likanifanya nifikirie sana, hivi kwenye ndoa mwanandoa akitaka kwenda mahali mfano mke amealikwa kwenye kitchen party, safari ya kikazi, safari ya kusalimu nyumbani, je anaomba ruhusa au anatoa taarifa mapema ili liwepo kwenye ratiba? Kama mke anapaswa kuomba ruhusa na anaweza kupewa au kunyimwa, mume je? Naye aombe ruhusa?

Advertisements

9 thoughts on “Kutoa Taarifa au Kuomba Ruhusa?

  1. asante womanofchist kwa bandiko hili zuri, kwa maoni yangu swala hili si la kulitazama kwa upande mmoja, kwani haliwezi kuapply kwa wanaume maana wao kuomba ruhusa kwa wenza wao huu ni msamiati mpya kabisaaaa! lakini hapa ni vema kutoa taarifa , hiyo ni alama nzuri inayoonyesha mawasiliano mazuri. namna hii itatoa picha kuwa wana ndoa ni wadau wenye hisa sawa katika ndoa yao hivyo kila mmoja anawajibika kwa mwenzie.

  2. Shalom! huyo baba hakutenda vyema,nadhani wanandoa wanapeana taarifa kama kuna tatizo wote wanakaa na kulijadili nini kifanyike na kutafuta muafaka sio kumkatalia kwa mabavu ni vizuri angemweleza alternative ukizingatia hyo pamoja na kuwa mama na mke bado ni sehemu ya familia huko atokako.

  3. Nadhani kuna wakati mwanamke anastahili kuomba ruhusa na kuna wakati anatoa taarifa, kwa mfano huu nadhani mume hakumtendea vema mwenzie, kwa sababu suala lilikuwa wazi kwa wote wawili, lilijulikana mapema, na pia mume angefikiria nafasi ya mkewe ktk familia (ya mkewe), hii yaweza hata kumjengea chuki kwa ndugu za mkewe.

  4. mi nafikiri hakutenda vyema,alipaswa kuelewa nafasi ya mkewe katika shughuli hiyo. wangekaa na kupanga wangepata soln ya suala la watoto. ila ni jmabo zuri na la kupendeza kupeana taarifa au kuaga. Mf mimi nikiwa hata na safari za kikazi huwa namtaarifu mwenzi wangu naye pia hufanya hivyo. Kwa mtazamo wanguni inategemea na life style ya wanandoa. Hekima ya Mungu itutawale

  5. Mimi naona ni vizuri kupeana taarifa mapema na kuangalia kama ratiba yenu kama wanandoa inaruhusu mmoja wenu kusafiri.Ila suala la kuomba ruhusa linaonyesha kuwa mwanaume ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho na hakuna kushauriana.

  6. wapendwa wamama wenzangu au wake au wanawake kwa ujumla swala sio kutoa taarifa tunatakiwa kuomba ruhusa akikunyima usilazimishe kwani hata mbingu na biblia inatambua kuwa mume ni mamlaka iliyo juu yako kabla ya Kristo yeye ni kichwa ni kama kabla ya kuolewa wazazi ndio mamlaka kuu wasipokubariki hivyo ndivyo, hapa ndio swala la meekness na humbleness linachukua nafasi ukijiwekea misingi ya kutoa tarifaa inaweza ikakusumbua huyu mama hakutakiwa kuumia bali kusubiri muda mzuri na muafaka na kuongea na mumewe na kuajaribu kuangalia ni jinsi gani mume wake anaelewa umuhimu wa kuhudhuria harusi na kujadiliana na kumuhakikishia jinsi gani watoto watukuwa chini ya unaglizi hata kama yeye mama akisafiri na kumkumbusha jukumu la ulezi kwani ingawa wababa wengi wanasema watoto ni kazi ya mama lakini malezi ni wote ni kweli imeandikwa kwenye mithali mtoto mwenye tabia mbaya ni mzigo kwa mamaye, dada mimi nikweli mume anamaamuzi ya ,mwisho hata unapoenda kanisani au kazini au popote lazima umuage ukienda na baraka zake unamshinda adui, shetani ametumia viburi vya wamama wengi hasa kuona sio sawa na ni haki yangu kuleta fujo kwenye ndooa nyingi sio swala la usomi au kutosoma kumuheshimu mumeo ni wajibu meekeness and humbleness is not a defeat rather a success njia pekee ya kum win mumeo ni kuwa hivyo mith 31 inajitosheleza lakini wanawake wa biblia utakumbuka vasti alinyang’wanywa umalikia kwa ujeri wa kukataa wito alipoitwa na mfalme hatimae Esta aliolewa na kuwa malkia mpya ni vyema kujua nafasi yako katika ndoa na wajibu, mume ni kichwa mke ni kiwiliwili (kinabii) kichwa hakiendi bila kiwiliwili sasa ukiona kila wakati unasema kwanini ameniambia hivi amenionea kwa vile yeye ni kichwa ujue unashida kwani kiwili wili kikitambua nafasi yake ndio kinaendesha kichwa na ndivyo ilivyo kichwa hakiwezi geuka bila shingo na ili kigeuke vizuri lazima mwili wote uangaie upande husika, asanteni-evodear11@yahoo.co.uk/Glory.

  7. Bwana YESU asifiwe! Wapendwa wanaume wenye tabia kama hizo wanapaswa kutubu,kwani wanatukwaza sana,pengine mtu umefiwa lakini hupewi ruhusa ya kuhudhuria msiba mpaka atakapopenda yeye kisa hawezi kukuruhusu uende peke yako mpaka uambatane naye kila unapoenda kwenye matukio jamani!!? huu ni unyanyapaa uliokithiri,wanaume ( baadhi ) muache mfumo dume lakini pia muwaamini wake zenu.

  8. shalom,imempasa mume kuishi na mkewe kwa akili.hapa kwa kutumia akili ya kawaida tu,mume angeangalia umuhimu wa mkewe kwenda harusini kisha wangeshauriana ni vipi pengo la kutokuwapo kwa mkewe lingezibwa.na kwa upande wa mama anapaswa kuona mbele kwanza kabla ya kuomba ruhusa mf.nitakapoondoka watoto nitawaachaje? watahudumiwa na nani wakati upi?sio kujali safari bila kujali familia yako kwa mipango.nafikiri angeandaa mazingira ya jinsi nyumba atakavyoiacha na akamweleza mumewe asingepata tatizo.kila mmoja ana nafasi ya udhaifu ktk hili.wakinamama tusimame ktk nafasi zetu kikamilifu na hawa wanaume pia ni wanadamu.

  9. shalom,imempasa mume kuishi na mkewe kwa akili.hapa kwa kutumia akili ya kawaida tu,mume angeangalia umuhimu wa mkewe kwenda harusini kisha wangeshauriana ni vipi pengo la kutokuwapo kwa mkewe lingezibwa.na kwa upande wa mama anapaswa kuona mbele kwanza kabla ya kuomba ruhusa mf.nitakapoondoka watoto nitawaachaje? watahudumiwa na nani wakati upi?sio kujali safari bila kujali familia yako kwa mipango.nafikiri angeandaa mazingira ya jinsi nyumba atakavyoiacha na akamweleza mumewe asingepata tatizo.kila mmoja ana nafasi ya udhaifu ktk hili.wakinamama tusimame ktk nafasi zetu kikamilifu na hawa wanaume pia ni wanadamu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s