Ongea Habari za Mungu kwa Watoto Wako

image

Shalom

Je Mungu ni sehemu ya mazungumzo yako ya kila siku na watoto wako? Au unakwepa kuongea nao habari za Mungu? Watoto wako wanamuona Mungu katika maneno yako ya kila siku? Kitu unachokithanimi utawekeza muda wako, mali na hata nguvu zako. Watoto wako waone jinsi unavyowekeza kwa Mungu katika kulisoma neno lake, kuomba, kuhudhuria kanisani na kutumika katika kazi ya Mungu.

Tunapozungumza ukuu wa Mungu na watoto wetu katika maisha ya kila siku tunawajengea hazina kubwa ya imani kwa Mungu wao ambayo watakuwa nayo siku zote. Pamoja na kuwahamasisha kupata maksi nzuri darasani, kujihusisha na michezo na kufanya kazi za nyumbani hakikisha unawafundisha kumtumikia Mungu katika umri wowote walionao. Neno la Mungu liwe sehemu ya maisha yako na watoto wako siku zote.

KumbuKumbu 11:18-19Kwa hiyo yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohonu mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. Nayo yafunzeni Vijana vyenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s