Usifiche Dhambi Mweleze Yesu

image

Moyo wako umekata tamaa, unajiona hufai kabisa mbele za Mungu. Ulikuwa mwaminifu sana ila sasa umeanguka na unaona aibu kuinuka na kutubu. Mungu anayajua maisha yako, sasa kwanini ujifiche? Mweleze kila kitu, sio kwamba hajui, la bali anataka kuona kuwa umejutia, umekiri na unahitaji rehema yake. Mungu ni mwaminifu, usikae na dhambi moyoni, mwambie Yesu.

Zaburi 51:1-12
“Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.
Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimeyajua mimi makosa yangu na dhambi yangu i mbele yangu daima.
Nimekutenda dhambi wewe peke yako na kufanya maovu mbele ya macho yako. Wewe ujulikane kuwa unahaki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu. Tazama, mimi niliumbwa katika hali ya uovu; mama yangu alinichukua mimba hatiani. Tazama wapendezwa na kweli iliyo moyoni; nawe utanijulisha hekima kwa siri,
Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko theluji
Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi.
Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu, uzifute hatia zangu zote.
Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.
Usinitenge na uso wako, wala Roho wako mtakatifu usiniondolee.
Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s