Thamani Yako Ni Kubwa Sana!

Shalom

Leo napenda nikukumbushe mwanamke / msichana kuhusu thamani kubwa uliyonayo. Gharama yake ni kubwa sana, Damu ya Yesu. Alikubali kuimwaga damu yake na kuvumilia mateso makali kwa sababu anakupenda sana na anakuthamini sana.

Usiruhusu mtu yoyote akushushe thamani na kukudharau kwa namna yoyote ile. Inasikitisha kuona binti anakuwa kwenye mahusiano na mtu anayemnyanyasa, kumuaibisha kwa maneno ya dharau na kejeli mbele za watu na hata kumnyima uhuru wake, na anaendelea naye tu. Mwingine anajua kabisa mchumba aliyenaye si mwaminifu na pia ni mgomvi, anampiga yeye bado anaendelea naye na wanafanya mipango ya kuoana kabisa.

Kumbuka kuwa wewe ni wa thamani sana, kuna watu wengi wanakupenda na kukujali mno na hawapendi kukuona ukiharibu maisha yako kwa kukaa na mtu asiyeijua thamani yako. Jithamini, tambua nafasi yako na kamwe usiruhusu mtu achezee maisha yako au hisia zako.

Advertisements

3 thoughts on “Thamani Yako Ni Kubwa Sana!

  1. Amen mtumishi wa Mungu leo nimebarikiwa sana na maneno hya. Kweli nimetambua mimi ni wa thamani kuliko nilivyojidhania. Mungu aendelee kutubariki.

  2. Akubariki sana Mungu ant yangu, unaelimisha jamii kwa maneno mazuri ya Mungu. Nimebarikiwa sana na ushauri wako. Wamaa wengi hawajui uthamani wao kwa Mungu hata kwa jamii pia na wana tabia ya kujidharau wenyewe, Mama jithamini wewe kwanza kwani usipojua kuwa wewe ni wa thamani ni vigumu kutegemea mtu mwingine akuone wa thamani. Jifunze kujinene mambo mazuri yenye baraka. Mama jacks Minja.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s