Msamaha na Uponyaji wa Moyo Baada ya Kutoa Mimba

image

Kutoa mimba ni jambo linalosikitisha na kuumiza sana, pale ambapo mtu pekee ambaye Mungu ameamua kuumba pamoja naye (mama) anapoamua kuukatisha uumbaji huo kwa sababu ya ubinafsi wake. Ni jambo linalomhuzunisha sana Mungu, na wanadamu pia na ndio maana hufanyika kwa kificho na halizungumziwi kwa namna yoyote ile. Ukimya huu huwafanya hata wale ambao wamegundua kosa waendelee kuishi katika majuto, maumivu na aibu kutokana na kukosa msaada wa kiroho.

Mtu anayesikia hukumu moyoni baada ya kutoa mimba hawezi kupata amanu hadi amepokea msamaa wa Mungu, na uponyaji wa roho yake ndipo ataweza kuachilia na kuwa mtu mpya. Ukweli ni kwamba, Yesu anaweza kukusamehe kabisa, na wala asikumbuke tena. Yesu alipokufa kwa ajili yetu, alichukua dhambi zetu zote haijalishi ni ya aina gani na kutuweka huru. Yesu anakupenda na kukujali, hivyo kama ulitenda kabla hujaokoka tambua ya kuwa ulipomkiri Yesu na kumpokea alikusamehe dhambi zako zote.

Isaya 1:18 “Haya, njooni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.”

Inawezekana umeshatubu na kumkiri Yesu lakini bado unaona hukumu juu ya jambo hili. Kwanza lazima ujisamehe, kubali kupokea msamaha wa Yesu na kujisamehe ili uweze kusonga mbele na kuachilia. Wokovu tunaupata kwa neema na wala so kwa matendo, Mungu hajakuchagua kwa sababu ya wema wako bali kwa sababu ya wema na rehema zake. Kubali upendo wa Yesu ndani yako na uishi kwa sababu ya neema yake.

Efeso 2:8 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu”

Kama hadi sasa bado hujampokea Yesu, au ulitoa wakati tayari unamjua Mungu, tumaini bado lipo. Tubu dhambi zako kwa Mungu kwa kumaanisha, mkaribishe Yesu upya ndani ya moyo wako na kubali kuishi katika pendo la Mungu na kumtazama Yesu siku zote na dhamiria kutorudi nyuma kamwe. Usijifiche kama vile upo saws wakati moyoni unaungua.

1Yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”

Kumbuka Mungu akikusamehe hatakumbuka tena dhambi zako. Kataa uongo wa shetani kuwa haujasamehewa, achilia na pokes msamaha wa Mungu na dhamiria kumfuata siku zote.

Ebrania 8:12 “Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, na dhambi zao sitazikumbuka tena.”

Ubarikiwe na Bwana Yesu.

Advertisements

11 thoughts on “Msamaha na Uponyaji wa Moyo Baada ya Kutoa Mimba

 1. thank you womenofchist,
  je mtu anapotoa mimba, ni lazima aongonzwe sara ya toba upya.

 2. Wow!!! Nimefurahi kuijua hii blog…. how comes sijaiujua miaka yote hii??? Ubarikiwe ili uendelee kutuhabarisha habari za wanawake wa Kikristo.

 3. Nimefurahi kuwa umeipenda blog hii, endelea kutembelea na waeleze na wengine pia.

 4. Mungu awabariki sana women of God. kila mara nimekuwa nikifuatilia blog yenu. nimejifunza mengi sana mimi kama binti. big up mummies

 5. jamani mungu awariki sana kwakutuletea hii blog kweli ni nzuri.mbarikiwe sana.

 6. Nimefurahi kuona blog yenu, je kama mtu akipata mimba nje ya ndoa na wanaishi na mwanaume hawajafunga ndoa, hapo afanyaje

 7. Karibu sana. Unaposhiriki tendo la ndoa unajua matokeo yake ni mimba hivyo unapoipata ni lazima uitunze hadi ujifungue kisha umlee mtoto. Uzinzi ni dhambi mbele za Mungu hivyo achana kabisa na Tania hizo na umrudie Mungu.

 8. Mungu awabariki sana Wanawake wa Mungu mchango wenu huu wa mafundisho unathawabu kwa Mungu

 9. womanofchrist

  Mungu awabariki sana kwa hilo watu wa mungu ni wadogo pale tu ambapo wanapotenda dhambi. Mchango huu ni mkubwa sana kwetu ss wanawake au mabinti wa YESU. UZINZI ni dhambi kubwa sana lakini si mimba zote ambazo mungu hupanga, kwamba lazima uwe mimba la!!!!!!!!!! MUNGU ATUBARIKI SOTE.

  Asemaye: Lucy kabuta

 10. God bless you woman of christ.Kutubia dhabi kama hiyo,nilazima ukaeleze kwa pst au mbele za madhabahu ndio usamehewe?ama kwa kusiki umemkosea mungu ndani yako kwa kuugua moyoni upige magoti na umulilie mungu hiyo mungu hawezi kusamehe?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s