Mume wa Mithali 31

image

Imezoeleka kuwa mtu akisikia kuhusu mithali 31 basi moja kwa moja anajua kuwa ujumbe huo unawahusu wanawake. Ni kweli kuwa mistari hii ni mahususi kwa ajili ya wanawake, ila pia ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke anayezungumziwa hapa ana mume.  Biblia haijatoa sifa za mchumba mwema bali mke mwema, na huyu mke mwema ameweza kuwa mwema sababu mumewe pia ni mume mwema. Kwa haraka sifa za mke mwema zilizopo hapa ni mchapakazi, mkarimu, mjasiriamali, anayejali, mtunzaji wa familia yake.

Mume wa mke huyu amezungumziwa pia kwa mema:
1. Mstari wa 11 “Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato”

Anamwamini mke wake. Sio kumtawala kwa mabavu wala kumhisihisi vibaya. Aliamini kuwa mke wake anamuwazia mema na nia yake ni kujenga familia bora na imara na sio kushindana naye. Alipomuamini mke wake, alimpa nafasi ya kuonyesha uwezo wake na hivyo familia kunufaika. Mwanamke aliyeolewa anahitaji kujiona anaaminiwa na mume wake ili aweze kukitoa kwa nguvu na uwezo wote katika kujenga familia imara.

2. Mstari wa 23 “Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.”

Ni mtu anayejishughulisha na masuala muhimu ya maendeleo ya jamii yake. Hafuati tu mambo yake mwenyewe bali pia maslahi ya jamii yake kwa kuketi pamoja na wazee wa nchi. Ni mtu anayeshirikiana na wengine.

3. Mstari wa 28,29 “Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu na kusema, Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.”

Anamsifia mke wake kwa yale anayoyatenda kwake na kwa familia nzima. Haoni aibu kumsifia mkewe. Mume huyu alionyesha kujali ma kuthamini mchango wa mke wake katika familia na akamsifia kwa hilo.

Ni muhimu kila mume akaiga mfano wa mume huyu:
– Anamwamini mke wake.
– Anajishughulisha na jamii yake, hajitengi na watu anaoishi kati yake.
– Anamsifia na kumthamini mke wake.

Advertisements

5 thoughts on “Mume wa Mithali 31

  1. Hi inaonyesha ni jinsi gani mwanamke anahitaji kupendwa na kutunzwa.muhimu ni upendo kati ya mke na mme.pia mke na mme wanahitaji upendo wa agape.

  2. Ni wanaume wachache wana tabia ya kusifia wake zao,wengi wao hata kama utacontribute vipi income ktk familia lakini wanaishia kunyanyasa tu wake zao kana kwamba walilazimishwa kuwaoa,Mungu awasaidie sana wanaume wa namna hii.Amen

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s