Usalama wa Watoto – Afya ya Dada wa Kazi

Shalom

Wote tutakubaliana kuwa kwa wengi wetu dada wa kazi anakuwa na mtoto mara nyingi kuliko mama yake hivyo ni muhimu sana sana kuhakikisha afya ya dada huyo ni njema kwa ajili ya usalama wa watoto. Ni wajibu wa mzazi kuangalia kama dada anaugonjwa wowote wa ngozi na kumpatia matibabu haraka iwezekanavyo kwa faida ya wote. Vile vile magojwa kama kikohozi na flu ni lazima kutibiwa mapema maana ni rahisi mtoto kuambukizwa.

Jambo lingine ni kuwa tufahamishane nini mzazi anapaswa kufanya anapogundua au kuhisi  kuwa dada wa kazi amepata maambukizi ya virusi vya ukimwi na wakati mwingine ameanza kuugua magonjwa nyemelezi? Tukubali kuwa siku hizi hali imebadilika sana, hivyo hatuwezi kufumba macho wakati tatizo lipo. Tushirikishane na kusaidiana katika hili wapendwa, ili tuweze kuwaepusha watoto wetu na hatari za kiafya.

Karibuni tusaidiane kwa mawazo….

Advertisements

One thought on “Usalama wa Watoto – Afya ya Dada wa Kazi

  1. Mimi nina uzoefu wa wifi yangu..alishawahi kukaa na msichana wa kazi mwenye VVU bila wao kufahamu na pia msichana mwenyewe hakujifahamu. Binti alikuwa anaumwa malaria mara kwa mara, magomjwa km kikohozi ambacho hakiishi..Kaka yangu alishauri afanyie check up. then ikagundulika ni muathirika…
    Haikuwa rahisi binti kujikubali, lakini alipewa ushauri masaa na akarudishwa nyumbani kwao. kaka alimpatia pesa ya kuanzisha biashara ili ajikimu kimaisha.
    Ni vizuri kuwa na utaratibu wa kuchunguza afya za wasichana wa kazi, ili kuepuka athari mbalilmbali.
    Asante womanofchrist.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s