Ujasiri: Mruhusu Yesu Atawale Maisha Yako

Shalom

Maisha ya mwanamke yanahitaji ujasiri wa hali ya juu sana. Kila siku ya maisha yetu tunakutana na mambo ambayo yanatuhitaji kuwa jasiri. Mambo mengine ni ya kawaida na mengine ni mazito sana. Inahitaji ujasiri kuamua kuondoka kwa wazazi wako na kuanzisha maisha na mtu mwingine wa familia nyingine, tamaduni nyingine, lugha nyingine na wakati mwingine nchi au taifa jingine! Ni ujasiri unaomuwezesha mwanamke kubeba mtoto tumboni kwa uaminifu kwa miezi tisa na kisha kumlea mtoto katika upendo na uvumilivu mkubwa. Unahitaji ujasiri kukabiliana na changamoto za ujana, changamoto za ndoa na pia malezi ya watoto. Na mengine mengi sana yanakuhitaji uwe jasiri ili uweze kukabiliana nayo mfano kufiwa, kupoteza kazi, magonjwa, n.k.

Mambo haya yote hatuwezi kuwa na ujasiri wa kukabiliana nayo hadi pale unapomruhusu Yesu aingie katika maisha yako na kushikilia usukani. Yesu anapoingia ndani yako anakupa utulivu wa moyo na ujasiri wa kukabiliana na yote yanayotokea katika maisha yako.

Marko 6:44-51, Hapa tunaona wanafunzi wa Yesu walimuacha Yesu akienda mlimani kuomba na wao wakaingia chomboni tayari kwa safari. Wakiwa katikati ya bahari mara upepo mkali ukakipiga chombo chao na dhoruba ikawa ya kutisha. Walitaabika sana maana Yesu hakuwa pamoja nao, baadaye Yesu alikuja na alipoingia ndani ya chombo upepo ukakoma na bahari ikatulia kabisa. Tunajifunza kuwa, tunapokutana na dhoruba kali maishani, uwepo wa Yesu ndio unaoweza kuzituliza. Mruhusu Yesu aingie ndani ya maisha yako ili aweze kutuliza dhoruba.

Ili uweze kuwa jasiri:

  • Mruhusu Yesu aingie ndani yako na ayatawale maisha yako.
  • Orodhesha maeneo katika maisha yako yanayokuletea hofu na wasiwasi.
  • Soma Marko 6:46-52 na ulinganishe na maisha yako na unayoyapitia.
  • Omba, msihi Bwana aingie katika mashua yako na kutuliza dhoruba.
  • Soma Zaburi 46:1-2, Uiweke moyoni na utafakari jinsi ya kuitumia mistari hii katika maisha yako.

Zaburi 46: 1-2 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima mioyoni mwa bahari.”

Advertisements

5 thoughts on “Ujasiri: Mruhusu Yesu Atawale Maisha Yako

  1. amina nami umenipa neno katika maisha yangu. lakini natamani kujua ni muda gani mnakuwa on line. naitwa Cecile Kalangu

  2. Bwana apewe sifa! samahani kukurudisha nyuma kidogo. naomba unitumie ratiba ya chakula ambayo utakuwa unatumia wewe ili nione kama nami itanifaa au ni badirishe wapi

  3. Mara nyingi mida ya asubuhi saa tatu hadi saba mchana na usiku saa mbili hadi nne

  4. nimependa sn jaman hii topic y watoto.mungu awabariki sn. mm nina watoto wawili.huyu mdogo ana miez 4. nahtaji kujua mengi kuhusu mtoto. anaanza kukaa n umri upi? n wakike

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s