Ujasiri: Simama Imara Katika Yesu Katikati ya Matatizo

Zaburi 27:3
“Jeshi lijapojipanga kupigana nami,
Moyo wangu hautaogopa.
Vita vijaponitokea,
Hata hapo nitatumaini. “

Unapokabiliana na hali ngumu na matatizo katika maisha yako, moyo hupata hofu na wasiwasi. Ili kuweza kuwa jasiri inabidi kusimama imara katika Yesu na neno lake. Kamwe usikate tamaa kwa sababu majaribu yamekuzunguka, kila mara kumbuka mistari hii ya Zaburi 27:3

Pia unapaswa kutokukata tamaa, usikate tamaa hata kama tatizo lako limechukua muda mrefu sana. Endelea kumwamini Mungu na siku yako ipo. Ukisoma Luka 8:43-48 na Marko 5:25-34 tunamuona mwanamke  asiyekata tamaa. Hakuangalia ukubwa wa tatizo lake, uwingi wa watu wala sheria za wayahudi bali alitambua nguvu na uwezo wa Yesu na hivyo aliamini kuwa atapokea muujiza wake.

Alikuwa ameshatumia mbinu zote ili kuweza kupata uponyaji na hakufanikiwa hivyo aliposikia Yesu anapita alifurahi sana akijua siku yake imefika. Alipoona umati mkubwa umemsonga Yesu hakukata tamaa bali kwa imani alisogea na kushika pindo la vazi lake na palepale akapokea uponyaji.

6 thoughts on “Ujasiri: Simama Imara Katika Yesu Katikati ya Matatizo

 1. Amen.
  Nimebarikiwa na hilo.
  Mungu azidi kukutumia, uzidi kututie moyo tuliokata tamaa.

  Be blessed.
  Neema.

 2. Amen Mtumishi wa Mungu ni kweli hatupaswi kukata tamaa,mwenyewe nimepitia magumu mengi lakini sikati tamaa nazidi kusonga mbele,mitihani ni sehemu ya maisha hata ukiangalia mitume walivyopata shida wakati wanamtumikia Mungu,lakini hawakukata tamaa walisonga mbele,mwendo waliumaliza,imani wakailinda,hivyo nasi inatupasa tuilinde imani,na mwendo tuumalize.Amen.

 3. inatupasa kutokata tamaa, japo yapo majaribu mengi tunapitia.be blessed kwa kutupa ushauri.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s