Mahusiano ya Kirafiki

Shalom

Wapendwa, ni mategemeo yangu kuwa mpo salama kabisa kwa neema za Mungu wa mbinguni. Leo tuangalie kwa ukaribu mahusiano ya kirafiki baina ya jinsia tofauti. Nikawaida kwa mdada kuwa na marafiki wa kiume, marafiki wa kawaida ambao mnaweza kuwa mnaabudu pamoja, mmesoma au mnasoma pamoja, mnaishi mtaa mmoja, n.k. Jambo hili sio baya maana ni sehemu ya maisha. Huwezi kuwakwepa maana hakuna ubaya juu ya kuhusiana nao katika hali ya kawaida. Tatizo likakuja pale ambapo msichana uliyeokoka unapomruhusu huyo rafiki yako awe huru na wewe kupita kiasi.

Mambo yafuatayo hayapaswi kabisa kwa binti aliyeokoka kuyafanya au kuruhusu kufanywa na marafiki wake wa jinsia tofauti.

1. Kumruhusu rafiki yako, hata kama ameokoka kukushika mkono wakati mnatembea (kutembea mmeshikana viganja), kukumbatiana na kubusiana mkiwa wawili/ mkiagana, kukupet pet (kukishika mgongo, miguu kama anafanya massage), na kushikana shikana kwa kupitiliza.

2. Kuwa mmeunganika kihisia kiasi kwamba huwezi kupitisha siku haujawasiliana naye, kumfanya yeye ndiye anayekufariji kihisia (nazungumzia rafiki asiye mchumba wako). Unaweza ukaunganika na mtu kihisia na ikakuletea shida baadaye utakapoolewa.

Hakikisha kila mtu unayekuwa karibu naye iwe shule, kazini, majirani n.k anafahamu kuwa wewe umeokoka na unamaanisha.

1 Timotheo 4:12
“Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.”

Advertisements

One thought on “Mahusiano ya Kirafiki

  1. amina tumwombe Mungu atusaidie sana hasa sisi mabinti kwani tunapitia vishawishi vingi sana bila yeye hatuwezi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s