Usafi wa Kihisia

Kila mmoja wetu anaffahamu umuhimu wa kujitunza na kuwa safi hadi pale atakapopata mwenzi wa maisha. Kujitunza huku maranyingi huishia kwenye mwili, leo naongelea suala ambalo wengi huwa hawaligusii kabisa lakini linamadhara sana, usafi wa kihisia.

Kujitunza kwa ajili ya yule ambaye Mungu amekuandalia aihusishi kujitunza kimwili tu, bali kihisia pia. Hii inahusisha kutunza moyo wako, mawazo, maneno na macho pia. Inamaanisha kuuhifadhi ule uhusiano wa karibu wa kihisia kwa ajili ya yule ambaye Mungu amemuandaa kwa ajili yako na si mwingine yeyote. Kuepuka muunganiko wowote wa kihisia ambayo kwa kawaida ni rahisi kutokea lakini inaumiza sana kuivunja.

Usafi wa kihisia linaonekana kama ni jambo lisilowezekana katika kizazi cha sasa, lakini fikiria: Mume wako atakapokuoa atajisikiaje akijua kuwa kuna mwanaume mwingine anafahau hisia zako za ndani, malengo yako, hofu zako na mawazo yako? Atajisikiaje kujua kuna mwanaume mwingine anakufahamu vizuri kuliko hata yeye anavyokufahamu? Au utajisikiaje kujua kuwa kuna msichana alikuwa nafanya mazungumzo marefu ya hisia na undani na mume wako kabla hajawa na wewe na anamjua mume wako kiundani kabisa?

Sio tu unautunza mwili wako, kuna mambo mengi ambayo unatakiwa uyatunze kwa ajili ya mume wako pekee, yeye ndiye awe wa kwanza na wa mwisho. Wasichana wengi hawaoni umuhimu wa jambo hili, wanaweza kuwa na uhusiano wa kihisia na mwanaume ambaye hata hawanampango wa kuolewa naye na wakati mwingine mtu huyo hata hajaokoka. Hii ni mbaya sana maana ile nafasi ya kwanza ambayo anapaswa akae mume wako anakaa mtu mwingine.

Hapa siongelei sheria za kufuata ili usije ukakosea bali kuamua kujitunza na kutunza hisia zako kwa ajili ya yule tu ambaye umehakikisha kwa maombi kuwa ndiye. Kama ulikuwa na mtu, ukajua kabisa ndiye huyo na ukawa na ukaribu naye wa kihisia lakini baadaye mambo yakaja kuharibika, angalia usiingie kwenye  mahusiano na mtu mwingine hadi utakapohakikisha umemtoa kabisa kwenye moyo wako. Bila kufanya hivyo itakuja kukuletea shida kwenye uhusiano wako mpya, hii inawezekana kwa maombi na kumshirikisha Roho mtakatifu ambaye pekee ndiye anayeweza kukusaidia katika hili.

Mambo ambayo unapaswa kuyatunza na kuyafanya / kumfanyia yule ambaye unahakika atakuwa mume wako na si  mwingine yeyote ni pamoja na:

 • Maneno mazuri ya kujali na kuonyesha kumpenda
 • Kutoa zawadi au kupokea zawadi
 • Kutazamana usoni kwa mapenzi
 • Mtoko wa pamoja (outing), kumbukumbu za pamoja
 • Meseji zenye hisia za upendo
 • Kumwambia I love you / I love you too
 • Kumpa moyo wako na kumruhusu aingie moyoni mwako
 • Mawasiliano ya mara kwa mara kuelezana kila kinachotokea katika maisha yenu.
 • Kuzungumza hisia zenu za ndani, malengo, hofu, historia n.k

Bila Roho mtakatifu kutuongoza hatuwezi kuyatenda mapenzi ya Mungu, mruhusu ayatawale maisha yako na moyo wako ili uweze kuwa mshindi na zaidi ya mshindi.

Ubarikiwe na Bwana Yesu!

Advertisements

6 thoughts on “Usafi wa Kihisia

 1. Thank you so much.Maana hata Biblia inasema “Linda sana moyo wako kuliko vyote ulindanyo maana huko ndiko zitokako chemchemi za uzima”

 2. Karibuni muendelee kujifunza, Witness karibu kuuliza maswali ili niweze kujua unataka niendelee upande gani nami nitafurahi kufanya hivyo. Ubarikiwe

 3. Mage, thank you for such powerful article. ni kitu ambacho ambacho wengi tunakisahau,tunamshukuru Roho anavyozidi kutufundisha kupitia wewe.

 4. Kwakweli umenena Jambo la msingi sana dada, .inatokea hiyo,hasa pale tunapofuata utandawazi sana, unakuwa close na mtu as if ameshajicomit kwako!

 5. Tunaathirika na uelewa wao mdogo, wanaweza kuongoza vizuri wanaume kimahusiano, nitachangia zaidi ktk wide frame.hini sm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s