Weka Nyumba Salama

image

Kila mtu anajisikia salama zaidi anapokuwa nyumbani kwake.Hivyo ni vizuri ukahakikisha kuwa nyumba inausalama wa kutosha kwa wote wanaoishi ndani yake kwa kuweka kila kitu mahali pake kwa usalama.

Jikoni

1. Hakikisha mikono / vishikio vya sufuria vinaelekea pembeni mbali na upande wa kupikia ambapo watu wanapita / unasimama.

2. Hakikisha sabuni zote na dawa za kufanyia usafi zipo mbali na mahali watoto wanafikia.

3. Nyaya zote za vifaa vya umeme kama birika, blender n.k ziwekwe mahali salama.

4. Watoto wasizoee kuchezea sufuria tupu maana wanawea chukua zenye moto au vitu vya moto bila kujua maana wamezoea kuzichezea.

5. Visu na vifaa vyote vyenye ncha kali viwekwe mahali salama mbali na watoto.

Bafuni

1. Hakikisha vyombo vyote vya kuwekea maji vina mifuniko inayofunga vizuri.

2. Kama baf lina ‘tiles’ weka mpira maalumu wa kusimamia ili mtu asiweze kuanguka akiwa bafuni.

3. Sabuni, dawa na vipodozi vyote viwekwe juu mbali na watoto.

Vyumbani

1. Usiweke dawa, vipodozi au hela za sarafu mahali ambapo watoto wanafikia kwa urahisi.

2. Watoto wenye umri chini ya miaka sita wasilale kwenye kitanda laini sana au chenye mablanketi mengi.

3. Nguo zote zenye kamba ziwekwe kabatini mbali na watoto. Hakikisha milango ya kabati imefungwa vizuri.

3 thoughts on “Weka Nyumba Salama

  1. Kweli nimefurahi kupata Elimu ya namna ya kuweka usafi nyumbani.

    Naomba kuuliza kwa nini watoto walio chini ya miaka ya sita wasilalie kitanda kilaini au chenye blanketi nyingi?

  2. Kitanda kilaini namaanisha kile ambacho anaweza kudumbukia katikati na kufunikwa na godoro. Ni hatari sababu watoto huwa wanageuka geuka na wana usingizi mzito hivyo ni rahisi kufunikwa na godoro au blanketi usoni na kukosa hewa.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s