Mfundishe Mtoto Kuomba

image

Shalom

Pale mtoto anapoweza kuongea ni wakati muafaka wa kumfundisha kuongea na Mungu wake. Usisubiri awe mkubwa ndio umfundishe kuomba, anza mapema kumjengea msingi imara wa maombi.

Mfundishe mtoto kumshukuru Mungu kwa mambo mbalimbali, afya, wazazi, toys, chakula, nguo n.k. Pia kumwomba Mungu pale anapopata hofu, huzuni au kuumizwa. Vilevile ajifunze kuwaombea wadogo na wakubwa wake, walimu wake, marafiki zake na majirani pia. Hii itamjengea pia upendo kwa watu ambao anawaombea. Mweleze kuwa Mungu anampenda na anasikia maombi yake na anapenda kuzungumza naye.

Omba naye wakati wa Kula, akiamka asubuhi, usiku wakati wa kulala, anapoondoka kwenda shule na pale unapomuombea mtu mwenye mahitaji. Pia umfundishe kumshukuru Mungu pale maombi yake yanapojibiwa.

Ubarikiwe na Bwana Yesu.

Advertisements

3 thoughts on “Mfundishe Mtoto Kuomba

  1. Asante kwa kutukumbusha mambo ya msingi kwa watoto wetu. Mungu awabariki sana

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s