Mke Kuwa na Kipato Kikubwa Kuliko Mume

Shalom

Baadhi ya familia mama ndiye mwenye elimu kubwa au kipato kikubwa kuliko baba. Mara nyingi hali hii haisababishi tatizo lolote pale ambapo kila mmoja anaifahamu nafasi yake.

Lakini tumeshuhudia matatizo mengi sana kutokana na jambo hili hadi baadhi ya vijana wa kiume wanasema hawawezi kuoa msichana aliyewazidi kipato au elimu. Je, nini hasa kinasababisha matatizo hapa? Ili familia ya aina hii iwe na mshikamano nini kifanyike?

3 thoughts on “Mke Kuwa na Kipato Kikubwa Kuliko Mume

  1. Kuna mambo matatizo mawili ya msingi ya kuangalia hapa. Kwanza ni upande wa mwanaume, katika mazoea ya wengi na saikolojia za wanaume wanapata ujasiri wanapoona kuwa wana uwezo zaidi ya mke wake hasa uwezo wa kiuchumi wachilia kuzidi elimu. Hata wengi tutakubaliana wakati wa kuoana wachungaji wanauliza kijana wa kiume anafanya nini na wanafundishi kuwa kibiblia mwanaume ndio wa kutunza familia. Sasa inapoonekana mke kutunza familia tayari inaanza kumpa shida huyu mme atakosa ujasiri na inaweza kuleta shida.
    Upande wa mke ni kuwa yeye naye amefundishwa kuwa atatunzwa na mme wake sasa anapoona sasa anamtunza mme inampa nae shida. Ndio maana kama mke anayo hekima akiona haya anabidi ajue namna ya kumsaidia mmewe. Tukatakubaliana kuwa ni rahisi sana mme kuoa mke ambaye hafanya kazi za moja kwa moja za kuingiza kipato na akatunzwa na mme wake na bila kulalamikiwe. Ila kwa wake wengi hata waliookoka mme wake anaweza akawa hana kazi miezi miwili tu mke ataanza kulalamikia jambo hilo. Utasikia pesa zangu zote zimeishia kwenye mambo yako. Hii inaumiza wanaume wengi.

  2. Ni kweli kabisa,mwanamke kama hana hekima akiwa na kipato kikubwa kuliko mmewe atataka kuwa mtawala/kichwa cha nyumba au controller wa nyumba which is against God’s rules.Na kwa asili yetu wanaume hatupendi kutawaliwa hasa na wake zetu so italeta shida tu.
    Ushauri wangu mwanamke hata kama una kipato kikubwa kuliko bwana wako ,jitahidi sana kumfanya mmeo awe controller wa kipato hicho..mwaweza fungua business akaisimamia ..na mambo yakawa mazuri.Katika mambo yote hekima ya MUNGU inahitajika sana katika jambo hili.Asante kwa mada hii.

  3. MKE NI LAZIMA AJISHUSHE SANA KWA MUMEWE.HAKUNA JAMBO LA KUSHINDIKANA. NDOA ITAKUWA NZURI TU. KWA UPANDE WA MWANAUME ASILEBWETEKE, AJISHUGHULISHE ILI ATOE MCHANGO WAKE KATIKA FAMILIA HATA KWA UDOGO NI YA THAMANI.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s