Wakwe

Shalom,

Leo nataka niongee na wanaume mliopo humu. Je mkeo akikwaruzana na ndugu yako na nduguyo akakuletea habari kuwa mkeo mbaya kafanya hili na lile, utamuuliza mkeo upate upande wake wa habari au utasimama na nduguyo kuwa mkeo mbaya na kakosea?

Ukijua kweli kakosea utasimama naye au utakuwa upande wa nduguzo na kumsema vibaya?

Wamama ambao mmekutana na jambo kama hili karibuni kutupa michango yenu ilikuwaje na nini kinapaswa kufanyika.

Advertisements

One thought on “Wakwe

  1. Shalom,

    Kwanza nianze kukupongeza kwa kuweka website hii yenye mafundisho mengi kwa sisi wakristo na hata kwa maisha ya hapa duniani. Sikupata kuijua awali mpaka leo nilipo google ili kutafuta kama naweza kupata maelezo ya bajeti ya nyumbani. Nimepitia kwenye ile bajeti uliyotengeneza 2010, imekuwa ni msaada mkubwa sana kwangu, na nafikiri mimi na mwenzangu tataanza kuitumia. Ubarikiwe sana.

    Swali ulilolituma hapo halina jibu la moja kwa moja. Iwapo leo ndugu yangu atakuja kuniambia ubaya wa mke wangu, inategemea na jambo alilonieleza, yeye mwenyewe mimi namchukuliaje, uhusiano wake na mke wangu ukoje ikiwa ni baadhi ya mambo yatakayonisukuma kwa hatua inayofuata. Hivyo katika mazingira fulani, naweza hata nisimuulize mke wangu na nikapuuza, lakini vilevile inaweza nikataka nimuulize mke wangu na kusikia upande wake wa maelezo.

    Iwapo maelezo ni ya kweli, na kosa liko kwa mke wangu, binafsi nitasimama kumueleza mke wangu kosa lake, lakini nitafanya hivyo kwa njia isiyo ya kumdhalilisha, ikiwezekana tukiwa wawili. Mke/mume ni muhimu kama alivyo ndugu, ila kwa mtazamo wangu ni kweli tu itakayotuweka huru, kwahiyo la msingi ni kuwa wakweli na kutenda haki katika kutoa maamuzi inapobidi kufanya hivyo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s