Kuwaombea Watoto

Shalom

Ni jambo la muhimu sana kuwaombea watoto wetu kila siku. Mara nyingi tumekuwa tukiwaombea pale wanapopata tatizo au kuugua na kusahau kuwa shetani anawawinda kila siku. Tunapaswa kuwaombea na kuwafunika na damu ya Yesu kila wakati.

Kitabu cha power of a praying parent kina muongozo mzuri sana wa namna ya kuwaombea watoto wetu. Nimeona wazazi tuliopo hapa tuwe na utaratibu wa kuwaombea watoto wetu kwa kufuata muongozo huu. Nitakuwa naweka kila siku nini la kuombea na mistari ya biblia ya kusimamia na kama kuna hitaji la ziada unaweza kutushirikisha.

Mungu atuwezeshe kuwaombea watoto wetu kwa uaminifu. Amen!

7 thoughts on “Kuwaombea Watoto

 1. Bwana Yesu asifiwe mpendwa.
  Nimefurahi sana kwa mada ya leo. Naamini itatusaidia wengi. Mara nyingi tumezoea kuwaombea watoto kipindi tu wanapopata matatizo. Sasa namshukuru Mungu nimepata nguvu ya kumwombea mwanangu kila siku.
  Naomba kujua mwandishi ni nani wa hicho kitabu na naweza kukipata wapi.

  Mungu akubariki.

 2. Bwana Yesu Asifiwe,
  Kwa kweli mada ya leo inapendeza. Maana wazazi tumekuwa wasaulifu kwa hilo, naomba Mungu atutie nguvu juu ya hili la kuwaombea watoto wetu.
  Mungu akubaliki mpendwa

 3. Mtumishi wa Mungu ubarikiwe kwa huduma hii..je hicho kitabu tutakipata je.mimi niko posta mpya jengo la Azikiwe floor ya Kwanza University of Dares Salaam Computing Centre

 4. Amen,
  Mimi sio mjuzi sana wa mitaa ya posta ila karibu na jengo la ttcl kuna round about maeneo hayo kuna bookshop inaitwa CLC vinapatikana hapo. Pia maeneo ya survey karibu na ESAURP kuna Christian bookshop pia vinapatikana

 5. Ubarikiwe sana kwa kutukumbusha kina mama.mi kweli tuna jukumu la kuwaombea watoto wetu.

 6. Ahsante kwa kutukumbusha kuwaombea watt wetu..Mungu atusaidie n kutupa nguvu ktk hili…

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s