Lishe ya Mtoto – Miezi 12-18

 

Kuanzia miezi 12 watoto wengi huwa wameanza kutembea na hivyo kuongeza michezo. Kutokana na kucheza zaidi watoto wanahitaji kula vizuri ili kuendeleza uzito na afya zao. Pia watoto wanakuwa wameota meno angalau nane hivyo wanaweza kutafuta chakula kilichopondwapondwa. Katika umri huu mtoto anaweza kula chakula chochote ambacho hana allergy nacho.

Ni vyema ukaandaa ratiba ya kumlisha mtoto wako na menu ya nini cha kumpa kila siku. Ratiba iwe mahali ambapo kila mtu anaweza kuiona kwa urahisi ili wote wanaohusika na malezi ya mtoto wajue nini mtoto anatakiwa kula na wakati gani. Kila siku hakikisha mtoto anapata vyakula kutoka kwenye makundi makuu ya vyakula; wanga, vitamini, protini na mafuta.

Vyakula kulingana na makundi haya ni kama ifuatavyo:

Wanga

 • Nafaka
 • Viazi
 • Ndizi za kupika

Protini

 • Nyama (Ng’ombe, Kuku, Mbuzi n.k)
 • Samaki
 • Mayai
 • Maziwa
 • Maharage na jamii yake

Vitamini

 • Mboga za majani
 • Matunda

Mafuta

 • Karanga
 • Ufuta
 • Siagi

Vyakula hivi vinaandaliwa kwa namna mbalimbali ili kuweza kuliwa  vizzuri na watoto. Nafaka kama mahindi, mtama, ulezi, mchele n.k unasaga unga kwa ajili ya kumpikia uji. Kwa sababu mtoto ameshakuwa kidogo ni vyema ukamsagia lishe (kuchanganya nafaka mbili au tatu pamoja na karanga au ufuta). Karanga unaweza saga ppamoja na nafaka au ukasaga mwenyewe kwenye mashine na kumwekea kiasi kila unapopika chakula chake. Viazi na ndizi hutumika zaidi kupikia mtori ukichanganya na vyakula vya protini (nyama, samaki, maziwa) na mbogamboga, vile vile unaweza weka kiasi kidogo cha njegere.

Protini (nyama, samaki) unachemsha vizuri na kumpa supu nzito isiyo na viungo vingi. Samaki tumia wale wakubwa wasio na miiba midogo midogo. Mayai unachemsha na kumpa kiini ukichanyanya na maziwa kidogo au unapikia yai kwenye uji. Mtoto wa umri huu hatakiwi kula zaidi ya mayai matatu ya kienyeji kwa wiki, usimpe mayai ya kisasa kabisa. Maziwa unamchemshia ya kunywa na vilevile unapikia kwenye chakula chake, usipike chakula bila kuweka maziwa fresh. Unaweza pia chukua wali uliopikwa, ukachemsha maziwa nakisha kusaga wali na maziwa kwenye blender na kumpa mtoto. Wali unaweza upika na karoti ili kuongeza virutubisho. Supu ya maharage yaliyochemshwa tu ukasaga kwenye blender na maharage kidogo ina virutubisho pia kwa ajili ya mtoto wako.

Vitamini mbalimbali zinapatikana kwenye mboga za majani na matunda. Mpikie  mboga na kumsagia kwenye blender na kumpa kama supu, au changanya aina moja ya mboga kidogo tu kwenye mtori wake nakusaga kwenye blender. Matunda hakikisha yanaandaliwa kwa usafi wa hali ya juu, saga kwenye blender na umpe kama uji mzito. Matunda kama papai, parachichi na ndizi mbivu sio lazima umsagie ila hakikisha unapondaponda. Unaweza kumtengenezea juice ila matunda bila maji ni mazuri zaidi. Mkamulie chungwa mara moja kwa wiki, machungwa yana asidi hivyo usimpe kwa wingi.

Usisahau kumpa maji ya kunywa yaliyosafi na salama. Usimpe soda wala juisi za kununua madukani, hazina thamani yoyote kiafya na kemikali zilizotumika hazifai kwa mtoto.

Nawatakia malezi mema ya watoto.

20 thoughts on “Lishe ya Mtoto – Miezi 12-18

 1. Hii nimeipenda sana dada. Natamani kina mama wote wenye watoto wajue na wazingatie mafunzo haya. Hongera sana, na Mungu akubariki uzidi kutupa elimu nzuri kila mara.

 2. Thax women of chrisr. Msaaada kwa mtoto wa miezi 3…ambaye ndo anataka kumuanzishia chakula. Nahital ushauri nianze na kipi….nitamuacha asubuh na kurud mchanacwa sa 9. 30 alasiri.
  Ubarikiwe.

 3. Tangu kuzaliwa hadi miezi sita mtoto anatakiwa kunywa maziwa ya mama tu, na kama unaenda kazini mtafutie maziwa ya formula kulingana na umri wake. Wengine hukamua maziwa yao na kuyahifadhi vizuri kisha mtoto anapewa hadi mama atakapotoka kazini. Kwa sasa usimwanzishie chakula chochote. Ukiona uzito hauongezeki vizuri ongea na mhudumu wa afya ukienda clinic atakushauri nini cha kufanya.

 4. Asante sana kwa mafundisho mazuri, vip kuhusu mtoto wa miezi 6,je naweza kumpa hiyo mfululizo wa chakula? Mama Ester.

 5. Lishe kwa mtoto wa miezi 6-12 ipo, itafute kny post za nyuma au search Lishe ya mtoto miezi 6

 6. Asante saaaaaaaaaana, Mungu akubariki kwa elimu nzuri. Ninakwenda kuifanyia kazi. Nina twins wana 12months

 7. Asante kwa elimu ila mtoto wa miezi 12 maziwa fresh anapewa kama yalivyo bila kuchanganya na maji kama inavyotakiwa kwa watoto chini ya miezi 12 sio? @womanofchrist

 8. Tunashukuru kwa elimu lakini naomba kuuliza maziwa fresh anayopewa kunywa mtoto wa umri wa miezi 12 yanakuwa dilluted kama yale ya mtoto chini ya umri huo au inakuwaje? @womanofchrist

 9. asante na mung akubaasante na mung akubaasante na mung akubaasante na mung akubarki

 10. Naomb mnisaidie mwanang ana miez kum na nane an uzit wa kg 10 lkn kila nimpimapo uzit aongezek nifany nn jaman.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s