Tuwajali Wasaidizi wa Nyumbani

Lazima tukubali kuwa wadada wa kazi za majumbani wanachangia kiasi kikubwa sana katika mafanikio yetu kikazi, kimasomo na kibiashara. Jana nilikuwa clinic nikaona jinsi watoto walivyo comfortable na dada zao na jinsi wadada wanavyowajali, nikagundua kuwa bila wadada hawa wengi wetu tungekuwa nyumbani grounded.

Ndio wapo wengi ambao sio wazuri lakini haituzuii kuwatambua wale wazuri na wema na kuhakikisha tunawasaidia kuwa na future nzuri. Wengi wa hawa wasichana wanakuja wakiwa hawajui kitu, so naive na rahisi kudanganywa lakini wengi wetu hatujawahi kuongea nao kuhusu ujana na majaribu yake, wanapokosea kutokana na kutokujua tunakuwa wakwanza kuwafokea na kuwafukuza kabisa.

Wengine hawajui mimba inapatikanaje, hawajui kuhusu ukimwi n.k. wengine tumejifunza mambo hayo shuleni, wao shule hawajaenda ni jukumu letu kuwafundisha ABC za ujana na majaribu yake. I haven’t done this yet, but its a challenge to all of us. Let us try to be more of a mother and less of a boss to these young girls.

This is one of my new year resolution..join me for a change!

Advertisements

2 thoughts on “Tuwajali Wasaidizi wa Nyumbani

  1. Shalom, nimekupenda kwa hiyo point uliyoisemea mama wa kristo. ni kweli kabisa wadada hawa wanakaa na watoto wetu vizuri kuliko sisi na muda mwingi wako nao hivyo tunatakiwa tuaenzi kwa vizuri zaidi tuwafanye kuwa zaidi ya ndugu zetu. hii ni kwa sababu mbali na kuwabeba watoto wetu lakini wao ndio wanaoushika uhai wa familia kwani kila kitu kiko mikononi mwao, na wengi wamejikuta wakipanga hata bajeti za nyumbani mabosi kazi yetu ni kutoa tu fedha. ninawaomba mabosi hasa wa kike tuondoe roho mbaya na kauli chafu za kuwadhalilisha hawa wadada kwani wengi wao wanatufanyia kazi nzuri sana. Pia nawashauri wamama wenzangu kuwa pale unapokaa na mtoto wa mtu zaidi ya miaka mitano hebu msaidie walau hata apate elimu ya ujasiria mali ambayo itamsaidia aikwa katika nyumba yake. Wishing you alll Merry Xmasss and prosperous New year 2013.

  2. Uko sahihi kimsingi
    Watu hawa wanahitaji kuelekezwa kadri mama anavyoweza
    Nasema mama kwa sababu ndo aapaswa kuwa karibu naye kuliko baba
    Pale inapobidi ndo baba anaweza kuingilia kati lakini ni jukumu la msingi la mama kuwa karibu naye akimuelekeza mamabo mengi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s