Kusaidia Ndugu Kwenye Ndoa

image

Shalom

Jambo hili limezua migongano mingi sana kwenye ndoa hadi kupelekea ndugu kuona kwamba mke au mume anamzuia ndugu yao kuwasaidia. Pia imeleta shida kwa wanandoa wenyewe kwa wenyewe. Tatizo maranyingi sio ndugu bali ni wanandoa, mmoja anapoamua kutoa msaada kwa ndugu wa upande wake bila kumshirikisha mwenzie.

Mume na mke ni mwili mmoja, haijalishi nani anakipato kikubwa, nani anafanya kazi au familia ipi inauhitaji mkubwa; haitakiwi na si sawa kwa mwanandoa mmoja kuwasaidia ndugu wa upande wake kimya kimya. Hili ni kosa ambalo limewagharimu wengi, mwenzio akigundua kuwa unasaidia ndugu zako hata kama ni kidogo kiasi gani bila kumshirikisha hatafurahia, ataumia kwa nini umemficha na atajiuliza ni mangapi mengine unamficha.

Usitoe chochote nje ya familia bila kumshirikisha mwenzi wako, kabla hujaamua kumsaidia mshirikishe mwenzi wako na kwa pamoja muamue msaada gani amtatoa na kwa kiwango gani na kwa muda gani. Pia kama mmeongea ikaonekana hamna uwezo wa kutoa msaada kwa wakati huo, usiende kusema mimi ningekusaidia lakini mwenzangu kakataa”,kwenye ndoa hakuna mimi na yeye bali wote ni mmoja hivyo mweleze hali hairuhusu kwa wakati huo.

Pia usimkaribishe ndugu kuja kuishi nanyi bila kuongea kwanza na mwenzi wako na mkakubaliana katika jambo hilo. Ni rahisi ndugu kusema nanyanyasika kumbe mwanandoa mmoja amechukua maamuzi ya peke yake na hivyo huyu aliyepuuzwa anamalizia machungu na hasira kwa ndugu aliyekuja. Matatizo mengi katika ndoa yatamalizwa kwa ushirikishwaji wa kina kwa wanandoa wote na kutokufanya jambo lolote bila kumshirikisha mwenzi wako.

2 thoughts on “Kusaidia Ndugu Kwenye Ndoa

  1. Ubarikiwe sana kwa ujumbe mzuri, nadhani hii itasaidia ndoa nyingi ambazo ziko kwenye migogoro kama hiyo. Ni kweli kabisa si jambo jema kwa wanandoa kufichana mambo kama hayo, ndo mwanzo wa kutoaminiana pale mwenzi wako atakapogundua. Ataamini kuwa yapo mengi unayoyafanya nje bila kumshirikisha na hawezi kuwa na imani tena na wewe, na hapo matatizo na migogoro vitaanzia hapo. Wanandoa kuweni makini sana tambua kuwa sasa ninyi ni mwili mmoja, pangeni mambo yenu pamoja. mimi Leonce Venance

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s