Matumizi ya Fedha

Shalom

Leo tuzungumzie mambo ya fedha kidogo.

Wengi wetu tunafanya kazi au biashara na tuna malengo mengi sana lakini tumekuwa tukikwamishwa na fedha. Fedha tunayoipata inaisha haraka bila hata kujua imetumikaje. Ni ukweli usiopingika wanawake wengi huwa hatuna bajeti ya matumizi ya kila siku na mwezi. Je, unajua kwa mwezi familia yako inatumia kiasi gani? Je, unajua kuwa ni mambo gani hasa yanakumalizia hela zaidi?

Ni mara ngapi umekutana na nguo, pochi au kiatu na hukuwa na bajeti ya kukinunua ila sababu imeipenda na kwenye pochi kuna hela unanunua. Na wakati mwingine usiivae kabisa na kuishia kujaza kabati. Nani hajawahi kufanya hivi?

Changamoto ya kwanza nakupa, kwa mwezi mmoja mfululizo, ukijiona umetamani kununua kitu na hakiko kwenye bajeti yako, ushinde moyo, na kisha hiyo hela ambayo ungeitumia kukinunua iweke kwenye bahasha. Baada ya mwezi angalia zimefika kiasi gani utajua unapoteza hela kiasi gani kwa manunuzi usiyoyapangilia.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s