Ndoa ni Kutoa na Kupokea

Wanawake ni wavumilivu na jasiri sana. Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa familia na ndoa nyingi sana zingesambaratika kama sio uvumilivu na ujasiri wa mwanamke. Uvumilivu huu unahitajika sana katika maisha, ili kuleta maelewano na maendeleo. Lakini pia uvumilivu huu ukifika mwisho madhara yake ni makubwa mno.

Je ni nini hasa kinasababisha uvumilivu ufike mwisho? Ni pale ambapo mwanamke anapotazamiwa kuvumilia kila kitu na hapo hapo asikosee hata chembe maana yeye hatavumiliwa. Wanawake wengi wamevumilia mengi mno na wanaendelea kuvumilia, tena si kwa kushurutishwa bali kwa upendo lakini wale wanaovumiliwa hawalioni hili na badala ya kuwasupport na kuwapunguzia yapasayo kuvumiliwa ndio wanayaongeza wakijua watavumiliwa.

Wanawake wanapoingia kwenye ndoa wanaambiwa na kila mtu, uwe mvumilivu, na kwa ukweli wanazingatia kwa bidii. Wanafundishwa kutoa, kutoa, kutoa ila hawafundishwi kupokea na hakuna anayemwambia kuwa anastahili kupokea furaha, upendo, heshima, uvumilivu, haki za ndoa n.k. Na mwanaume anafundishwa kupokea furaha, kupokea matunzo, kupokea heshima, kupokea haki za ndoa, uvumilivu n.k. Yule anayetoa bila kupokea automatically itafika mahali ataishiwa vya kutoa maana havijalizwi na hapo utasikia mke wangu kabadilika, siku hizi hafanyi moja, mbili, tatu… Jiulize, atawezaje wakati akiba yake imeisha na mumewe haijalizi?

Nijuavyo ndoa ni kutoa na kupokea, kwa kufanya hivi akiba ya wote haitapungua na kamwe hautaona kama mtu amebadilika, maana mnajaziliza kila mmoja alipopunguka.

Advertisements

One thought on “Ndoa ni Kutoa na Kupokea

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s