Kuvunja Uchumba

Nawasalimu katika jina la Bwana,

Kuna jambo ambalo limekuwa likuwasumbua vijana wengi walio okoka, jambo hilo ni kuvunjika kwa uchumba. Napenda wote kwa pamoja tuongelee jambo hili ili tuweze kuelimishana na kusaidiana. Ni mara nyingi inatokea kijana akamwendea msichana na kumweleza nia yake ya kutaka kumuoa na msichana akakubaliana naye, wakaendelea kuwa wachumba kwa muda fulani kisha ghafla msichana akasema amegundua huyo sio mume sahihi na baada ya muda mfupi akawa na mchumba mwingine. Vivyo hivyo kwa kijana wa kiume kumuacha mchumba wake kwa ajili ya mtu mwingine.

Hali hii imekuwa ikiacha majonzi mazito kwa yule anayeachwa. Wengi wameumizwa hadi kufikia kumuacha Bwana, je hali hii hutokana na nini na nini kifanyike ili kuepuka watu kuumizwa kila mara? Na wakati mwingine unakuta binti anamwambia kijana subiri nitakupa jibu na anakuwa naye kwa zaidi ya mwaka bila kumpa jibu la ndiyo au hapana na huku akionyesha kuwa kama amekubali na baadaye anakuja kutoa jibu la hapana.

Utakuta pia kijana wa kiume anakuwa karibu sana na msichana fulani na kumuonyesha upendo wa ziada hadi yule msichana anadhani kuwa yule kijana anataka kumchumbia na pale anapomchumbia mtu mwingine inakuwa ni maumivu sana kwa yule aliyekuwa karibu naye kwa kila kitu. Sasa nini kifanyike ili kupunguza mambo kama haya.

Advertisements

2 thoughts on “Kuvunja Uchumba

  1. Tumsifu Yesu Kristo.Ndugu zangu katika Kristo,baada ya makubaliano ya uchumba,mumshirikishe M/Mungu kwa sala ili kama kuna tabia itakayojitokeza ndani ya ndoa yenu,isiwepo,napia kama kuna vishawishi vya kishetani,avivuruge kabisa.Kisha,jaribuni kuwaunganisha wazazi wenu wa pande zote mbili,kwani wao ni ni funguo katika maisha yenu kabla ya ndoa yenu.

  2. Kitu cha muhimu hapo ,ni vijana wajifunze kumsikiliza Bwana ili amani ya Kristu iamue ndani yao. Ni ngumu kutambua kile kilichomo ndani ya mwanadamu,Kufunga na kuomba ni jambo muhimu sana katika kutoa maamuzi mazito ambayo yatakufaidisha maisha yako .Vinginevyo utaishia kuumia.Vijana wasiwe na haraka ya kutoa maamuzi kwani ndoa ni jambo la maisha .Waepuke dhana ya kuwa kuoa/kuolewa ni kama fashion.Yaani mbona rafiki yangu kaolewa /kuoa? Pia tatizo kubwa la siku hizi vijana hawawashirikishi wazazi /wakubwa kwa ushauri zaidi mwanzo kabisa .Wazazi/walezi wana nafasi kubwa sana katika kushauri juu ya jambo kama hili.Ndio maana huwa kunakuwa na mshenga ambaye anapaswa kuwa mtu mzima.Vijana watambue kuwa furaha katika maisha inachangiwa na kuwa na ndoa bora.Utakuwaje na amani na furaha maishani kama ndoa yako haina furaha? Ndoa ikiwa ya amani na furaha hata kutumika kwa Bwana ni rahisi na Mungu anawabariki kama mwili mmoja.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s