Maombi

Shalom,

Nimepokea ombi hili, kwa pamoja tuombe Mungu aingilie Kati na katika hitaji hili.

Bwana Yesu apewe sifa.

Naomba kuleta maombi yangu: Dada yangu ana mimba yapata miezi saba. Lakini juzi amefanyiwa Ultra -Sound ikabainika kuwa mtoto ana matatizo. Ubongo wa mtoto haujafunga, aidha wamemwambia kuwa hata kama mtoto atazaliwa hataishi. Amechanganyikiwa na amekosa ujasili.
NAOMBA watu wa MUNGU tumuombee
(i) Awe na amani moyoni mwake na aweze kulipokea jambo hilo. (ii)Tumuombee mungu afanye jambo juu ya mimba hiyo kwani hizo ni hila za shetani, ili aweze kujifungua vizuri na mtoto awe salama. Tunaomba hayo na kuamini katika Jina la YESU aliye hai AMINA!

Advertisements

2 thoughts on “Maombi

 1. Shalom mtumishi wa Mungu.

  Asante kwa kutushirikisha hilo pia, tutaomba Mungu aingilie kati katika hili katika Jina la Yesu……Ameeen!

 2. Pole sana mpendwa,

  Neno la Mungu linasema kwenye Isaya 66:6 “Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema Bwana; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako”. Kumbuka Mungu analiangalia neno lake apate kulitimiza (Yer. 1:12b)

  Pamoja na sisi kumsihi Mungu aingilie kati kumponya mtoto aliye tumboni, mimi naomba unapofanya maombi utumie mistari niliyotumia hapa kwenye jamvi hili kuomba “kwakuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu” (Lk. 1:37)

  Yeye Muumba wetu anasema “Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?” (Yer. 32:27).

  Kinachohitajika kwako ni imani kwa Mungu kwamba atatenda. “Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu (Math. 17:20).

  Kumbuka dada, imani yako itauambia mlima (ambao ni ubongo wa mtoto ulio nje) ondoka hapa urudi katika nafasi yako – kwa jina la Yesu Kristu wa Nazareth, na jambo hilo litatendeka. “Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng’oka, ukatupwe baharini, litatendeka ” (Math. 21:21). Muhimu usiwe na shaka moyoni mwako.

  Naomba niseme na wewe sala hii:

  Bwana Yesu, ninakuja kwako, mimi mjakazi wako nisiye stahili, ninakushukuru kwa mema mengi unayotutendea. Kwa namna ya pekee ninakushukuru kwa ajili ya dada yangu ___________ ambaye umemtumia kufanyika chombo cha uumbaji, na ukampa uja uzito wake kama alivyotamani.

  Ninaomba msamaha kwa makosa yote niliyokukosema mimi binafsi kwa mawazo kwa maneno, kwa matendo na hata kwa kutokutimiza wajibu. Ninaomba toba kwa makosa aliyofanya dada yangu ambayo yamekuwa chanzo cha tatizo la ubongo wa mtoto wake kutokeza nje. Ninaomba msamaha Ee Mungu kwa makosa ya familia, jamii na ukoo ambayo yanarithishwa kwetu. Ninasihi huruma yako ukatuoshe kwa hisopo, ukatutakase katika jina la Yesu.

  Baba ulisema, kwenye Isaya 66.9 kwamba, huwezi kuleta wana karibu na kuzaliwa, usizalishe na kwamba huwezi kulifunga tumbo la anayetegemea kuzaa. Ninakusihi Mungu, wewe usiyeshindwa jambo lolote, ukamguse mtoto aliye tumboni mwa Dada yangu ili ubongo wa mtoto ukapate kurudi sehemu yake, katika jina la Yesu. Mlinde mtoto, mtakase na mponye na kila roho ya kumfuatilia, ili atakapozaliwa, sifa, shukrani, utukufu, enzi na mamlaka vikawe kwako katika jina la Yesu.

  Asante Yesu kwa sababu umesikia na utakwenda kutenda sawasawa na haja za mioyo yetu. Asante Yesu kwasababu utakwenda kumpomya mtoto na Mama katika jina la Yesu Kristu wa Nazareth nimeomba na kushukuru – Amen.

  Mungu akubariki sana.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s