Mungu Anasamehe Kabisa

Unaona kama makosa uliyoyafanya mbele za Mungu ni makubwa sana, hayawezi kusamehewa. Umekosa ujasiri wa kusimama mbele za Mungu. Ulikuwa unamtumikia Mungu na kuhudumu madhabahuni, lakini sasa umemkosea Mungu na jambo hili unaliona kubwa sana huwezi tena kuhudumu. Umetubu, tena kwa machozi lakini unaona kama bado inakufuata.

Usikubali shetani akudanganye, Mungu anasamehe kabisa pale unapotubu kwa moyo uliopondeka.

1 Yohana 1:9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, kutusafisha na udhalimu wote.

Isaya 1:18 Haya, njooni, tusemezane, nasema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama.bendera, zitakuwa kama sufu.

Kila dhambi inamatokeo yake, na mara zote sio mazuri. Lakini dhambi husamehewa, hata kama matokeo yanabaki hiyo haimaanishi kuwa haijasamehewa. Mfalme Daudi alitenda dhambi ya kuzini na mke wa Uria, akatenda nyingine ya kupanga Uria auawe. Matokeo ya dhambi yake mtoto aliyezaa na mke wa Uria alifariki. Lakini Daudi alipotubu kwa machozi alisamehewa na akawa mfalme mkubwa hadi Yesu akazaliwa kwenye uzao wake.

Yesu aliwasamehe waliomtesa na kumtundika msalabani, kosa lako ni kubwa kiasi gani asisamehe?

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s