Tunda la Roho – Amani

Tumekwisha kuangalia upendo na furaha, leo tunaendea na somo letu la tunda la roho kwa kuangalia Amani.

Amani ya kutoka kwa Mungu haitokani na mazingira tunayopitia au mambo tunayokutana nayo. Amani ya Mungu huja kwetu na kudumu bila kujali tunapitia hali gani. Amani hii inatokana na kuwa na uhusiano mzuri na Mungu, kitambua kuwa siku zetu zipo mikononi mwa Mungu, na kufahamu kuwa Mungu ndiye mpaji wa vitu vyote. Amani hii ni matokeo ya moyo uliotulia mbele za Mungu.

Haimaanishi kuwa hakuna matatizo, ila amani ya kristo inakuwepo pale unapoamini kuwa Mungu yupo katikati yako hata unapopita katika matatizo. Ni lazima uwe na imani timilifu kwa Mungu, na kumtegemea yeye pekee.

Isaya 26:3 Utamlimda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu kwa kuwa anakutumaini.
Pia unapolifuata neno la Mungu utapata amani ya kweli.
Zaburi 119:165 Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza.
Neno la Mungu linaondoa hofu na wasiwasi na kukupa amani ndani ya moyo wako. Roho mtakatifu hutufariji na kutupa amani katika magumu tunayoyapitia.

Unapokutana na jambo linalokukosesha amani, kwanza omba kwa Mungu akujalie amani yake ipitayo akili zote. Tambua ukuu wa Mungu, uwezo wake, upendo na uaminifu wake. Yeye anauwezo wa kukupa amani ya kweli siku zote na katika hali zote.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s