Tunda la Roho – Uvumilivu 1

Uvumilivu ni hali ya kutulia na kungoja kwa saburi, kuchukuliana kwa upendo, kutazamia kwa kutokukata tamaa na kutokurudisha baya pale unapotendewa. Uvumilivu lazima uendane na huruma (kumhurumia yule anayekutendea mabaya) na kutokuwa na kisasi.

Uvumilivu sio tu kumngoja Bwana, bali kungoja huku ukiomba. Hana alikuwa mvumilivu, alimngoja Bwana ajibu hitaji lake huku akiomba. Alimvumilia penina aliyekuwa akimcheka kwa sababu ya kutokuwa na mtoto, hakugombana naye bali aliendelea kumngoja Bwana kwa maombi. Uvumilivu ni kukaa mahali ulipo na kungoja na sio kutangatanga huku na kule. Kuamini kuwa Mungu anakwenda kujibu mahitaji yako na kuendelea kuomba.

Tunapaswa kujitahidi kwa bidii kuwa na uvumilivu. Watu wa dunia huu wamekosa kabisa uvumilivu, kila mmoja anataka spate kwanza na awe zaidi ya mwingine. Uvumilivu unakutaka kuwatanguliza wengine. Ni wa muhimu sana katika mahusiano yetu na wenzi wetu, wazazi, watoto, majirani, kanisani, ndugu, kazini n.k. Tusiwe wepesi kuhukumu bali tuchukuliane na kuvumiliana kwa upendo.

1 Petro 2:23 “Yeye alipotukanwa hakurudisha matukano; alipoteswa hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.”

Yakobo 5:7 “Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s