Tunda la Roho – Utu Wema

Utu wema ni hali ya kujali wengine na kuguswa na yale wanayoyapitia. Ni hali ya kuona kuwa jirani yako ni sawa na wewe hivyo anapopitia magumu upo tayari kushiriki pamoja naye kwa upendo. Kupalilia utu wema yakupasa kuwapenda wengine kama unavyojipenda, kujali furaha ya wengine, kuwaona kuwa nao ni wa muhimu na kuachana kabisa na magomvi.

FLP. 2:3-5
Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;

Utu wema unaonekana katika kujali, kumuwazia mwingine mema, kuona hitaji la mtu na kumsaidia pasipo kuombwa au kuambiwa. Tunaona mfano wa dorkasi na mwanamke mshunami, walitoa msaada pasipo kuombwa bali kwa kutambua uhitaji wa watu. Matendo 9:36-42.

Ni ngumu sana kumtendea wema mtu aliyekutendea mabaya, ila kwa msaada wa Mungu tunaweza yote. Ombea adui zako na wale wote wanaokutendea mabaya, utaona kuwa huwezi tena kumuwazia mabaya mtu unayemuombea Mungu ambariki. Muombe Mungu akusaidie usiwe na chuki wala hasira juu ya watu waliokutendea mabaya. Yesu alikuwa mwema sana, jifunze kupitia maisha yake (somo la maisha ya Yesu litafuata baada ya hili).

Ujulikane kama mtu mwema na mfariji na sio anayevunja watu moyo.

Advertisements

One thought on “Tunda la Roho – Utu Wema

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s