Tunda la Roho – Fadhili

Utu wema hausimami peke yake, unasimamishwa na fadhili. Utu wema ni hali ya kujali na fadhili ni vitendo vya kuonyesha kujali. Mungu ni mwenye fadhili nyingi, hutufadhili kila siku hivyo nasi tunapaswa kuonyesha fadhili kwa watu wote. Jambo hili ni la muhimu sana, ulimwengu umejaa watu wabinafsi na wasiojali hivyo sisi tulio watoto wa Mungu ni lazima tuonyeshe tofauti.

Ni rahisi sana kuonyesha wema na fadhili kwa wale unaowapenda na kuwajali, ila ni kwa msaada wa Roho mtakatifu pekee unaweza kuonyesha fadhili kwa wale waliokutendea na kukunenea mabaya. Hapa ndipo tunapotakiwa kufika, kuwa na uwezo wa kuonyesha fadhili kwa wenye uhitaji bila kuombwa wala kuangalia utapata nini kutoka kwao. 1Tim 5:9-10, 1 Tim 2:9-10

Tujulikane kwa wema na fadhili tunazozionyesha kwa watu zaidi ya mavazi na muonekano wa nje. Biblia inamifano mizuri ya wanawake waliojulikana kwa jinsi walivyowafadhili watu wenye uhitaji, bila kutazamia malipo au sifa. Kwanza tunamuona Dorkasi aliyejihusisha na mahitaji ya wajane, aliwavika bila kutarajia malipo(Matendo 9:36). Kisha tunamuona mwanamke mshunami aliyetambua uhitaji wa Elisha na kumpatia hifadhi na kumhudumia bila kuombwa (2Wafalme 4:8-10). Vilevile Lyidia alipomwamini Yesu akaona Paulo na wasaidizi wake hawana mahali pa kupumzikia akawakaribisha kwake (Matendo 16:15). Mifano ni mingi sana, nawe Je ikitakiwa Mifano wa wema na fadhili iandikwe kwa kuwafundisha wengine kutoka katika maisha yako utapatikana?

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s