Tunda la Roho – Uaminifu

Uaminifu. Kusimamia lile unaloliamini na kulikiri bila kuyumbishwa na mtu, watu au hali. Kuwa tayari kupigania kile unachokiamini ambacho ni Mungu na neno lake. Mungu wetu ni mwaminifu, mwaminifu kwa neno lake na kwetu pia.

Mtu mwaminifu ni mtu anayeaminika kwa maana anasimamia lile analolikiri. Anafanya lile analiahidi, anasema anachomaanisha kutoka moyoni, anakamilisha lile analilolianzisha na pia kutumia muda na vipawa vyake vizuri. Mfano ni wale watumwa wawili waliotumia talanta zao vizuri kwa uaminifu. Mathayo 28:18-25

Mtu asiye mwaminifu hawezi kuaminika maana maranyingi analolitenda sio analoliamini, anabadili kauli kutokana na mazingira na ni mvivu. Ili uweze kuwa mwaminifu ni lazima ujawe na nguvu za Roho mtakatifu na usimame katika neno lake. Pia kumtafuta Yesu na kuenenda kama yeye alivyoenenda alipokuwa duniani. Aliifanya kwa uaminifu kazi aliyotumwa na baba yake na aliyavumilia mateso yote kwa uaminifu mkuu.

Uaminifu unaanzia katika mambo madogo. Kuwahi kazini, kufanya kazi kama inavyopaswa hata kama hakuna mtu anayekusimamia au kukukagua, kutenda Yale ambayo Mungu amekuagiza kuyatenda, kutumia kipawa chako kwa ajili ya utikufu wa Mungu.

1 TIM. 3:11 Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.

LK. 16:10 Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s