Tunda la Roho – Upole

Tunda la Roho – Upole

Tusichanganye upole na ukimya. Ukimya unaonekana kwa nje bali upole unaanzia ndani ya moyo. Upole ni hali ya kuwa na unyenyekevu wa kutoka ndani. Ni kutambua kuwa Mungu anayepigana vita vyetu hivyo sisi hatupaswi kuwa wagomvi wala wenye visasi bali wenye kuachilia na msamaha. Badala ya kutafuta kushindana, upole unatafuta kimbilio chini ya ngome imara Yesu Kristo.
ZAB. 60:12
“Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.”

Yesu alikuwa mpole na mnyenyekevu wa moyo maana alimwamini baba yake kuwa ndiye kiongozi wa maisha yake na anauwezo wa kukabiliana na chochote atakachokutana nacho njiani.

Upole unapatikana katika imani, imani ya kumwamini Mungu. Katika utii wa neno lake, katika kukataa magomvi na hasira, kuwa na moyo wa rehema na msamaha na kukataa kuwa mtu mwenye visasi, malalamishi na kujikweza. Ukitambua jinsi ambavyo hukustahili kusamehewa lakini Mungu amekusamehe, utaweza kupalilia upole katika maisha yako.
1Petro 3:4 “bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo na thamani kuu mbele za Mungu.”

Kung’ang’ania kuwatendea wengine vibaya kwa sababu tu wamekuumiza ni kukosa roho ya rehema na neema ambayo kwayo Mungu amekurehemu. Umepata msamaha bure nawe toa bure. Upole haumaanishi kuwa hauna nguvu, bali unanguvu za kuzitawala hisia zako na kuchagua kutenda mema.

Mithali 15:1 “Jawabu la upole hugeuza hasira; bali neno liumizalo huchochea gubu.”

Advertisements

One thought on “Tunda la Roho – Upole

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s