Kutendea Kazi Somo la Tunda la Roho

Baada ya somo ili wanafunzi waweze kujua ni kwa kiasi gani wameelewa somo mwalimu huwa anatoa mazoezi ya kufanya na baadaye mtihani. Sasa leo natoa mazoezi ya kufanya kwa kila mmoja wetu ili kuelewa zaidi somo na baadaye mtihani. Kama una swali lolote uwe huru kuuliza.

1. Tafuta mtu katika maisha yako ambaye hategemei kabisa wema kutoka kwako na umfanyie tendo la wema (mtu ambaye hamjazoeana, aliwahi kukukosea, anakuhisi labda upo juu sana). Mfano kumpeleka saluni ya kisasa ambayo hajawahi kuwaza kwenda, kumsaidia kuuguza, kumtia moyo katika magumu anayoyapitia, kumtoa out n.k kama Roho mtakatifu atakavyo kuongoza.

2. Amgalia mtu mwenye uhitaji na umtendee fadhili kulingana na uhitaji wake. Angalia lile ambalo ni uhitaji wake mkubwa na lipo kwenye uwezo wako. Mfano kumnunulia nguo za mtoto, kumlipia ada ya shule ya mtoto, kumfanyia shopping ya mwezi, kumnunulia nguo maana anavaa moja kila siku, kumpa ushauri wa kitaalamu bure n.k.

3. Angalia mambo Yale uliyoyapanga kuyatenda katika maisha yako na uliyokubali kushiriki na utathmini uaminifu wako. Mfano maombi binafsi ya kila siku na kusoma neno, maombi binafsi na ya kikundi ya kufunga, kwaya, uanachama wako katika chama au kikundi chochote, kuendeleza au kuanzisha biashara yako, kumtumikia Mungu kwa kipawa alichokupa, n.k. Kumbuka kuwa mkweli na nafsi yako.

Andika kila kitu kwenye diary au journal yako, ufanye kwa uaminifu utaona jinsi Mungu atakavyokufundisha kwa vitendo. Baada ya zoezi hili, mtihani unakuja.

Kumbuka:  “Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa Jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.” Ebrania 6:10

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s