Kumfundisha Mtoto Kazi za Nyumbani

Shalom

Ni vyema kumfundisha mtoto wako kazi mapema ili awe mtu mzima mchapakazi na mwenye bidii. Kazi zinaendana na umri maana lengo sio kumuumiza bali kumsaidia akue vizuri.

Miaka 2-3
1. Kutoa vyombo vyake anapomaliza kula
2. Kukusanya na kuhifadhi toy zake kabla ya kwenda kulala.
3. Kuweka nguo chafu alizovuliwa kwenye tenga la nguo chafu.

Miaka 4-5
1. Kupanga vitabu na madaftari yake mahali pake
2. Kufuta vumbi kwenye sehemu anazofikia.
3. Kudeki chumbani kwake na kibarazani.
4. Kumwagilia maua ya kwenye makopo.

Miaka 6-8
1. Kufua chupi na soksi zake
2. Kukunja nguo zake na kuweka kabatini
3. Kuandaa meza
4. Kufagia nje na kureki majani yaliyoanguka
5. Kuosha chombo chake baada ya kula
6. Kutandika kitanda

Miaka 9-12
1. Kufua nguo zake na kuanika
2. Kusaidia kuosha gari
3. Kumwagilia bustani
4. Kuhudumia mifugo
5. Kupalilia bustani na maua

Huu ni mfano wa kazi kulingana na umri. Wa umri mkubwa anafanya zote za umri wa chini yake na za umri wake. Kama kuna ambayo nimeisahau unaweza iweke hapa ili tuzidi kujifunza pamoja.

Advertisements

One thought on “Kumfundisha Mtoto Kazi za Nyumbani

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s