Funga Kurasa ya Zamani Fungua Mpya

Inawezekana kuna mtu mlikutana mkapendana na mkaahidiana kuoana. Mapenzi yenu yalionekana ni ya kweli na kila mtu wako wa karibu alijua. Baadaye bila sababu yoyote ya msingi akakuacha na sasa yupo na mtu mwingine na wamefunga ndoa. Umekata tamaa, umejaa uchungu na unamchukia huyo mtu aliyenaye sasa hivi.

Tambua kwamba huwezi kufungua ukurasa mpya kama bado umeng’ang’ania ukurasa wa zamani. Dhamiria kumtoa kabisa mtu huyo moyoni mwako, sio wako tena na huwezi jua Mungu amekuepusha na nini kwa kumwacha aende. Usiendelee kukaa katika past, samehe na kusahau kabisa na kusonga mbele. Usijinyime furaha ya maisha kwa sababu ya kuachwa maana huyo aliyekuacha anaendelea kufurahia maisha.

Roho mtakatifu ndiye anayetuwezesha kusahau magumu na kusonga mbele, mkaribishe katika maisha yako.

Advertisements

6 thoughts on “Funga Kurasa ya Zamani Fungua Mpya

 1. Hongera kwa kutoa mada mbalimbali za kiroho. Kwa upande wangu huwa zinanisaidia sana.
  Mimi ni mke na mama wa mtoto 1 mwenye miez 11. Ndoa yangu ina mwaka na miezi 10 sasa. Mume wangu ni mtu mzima na amenizid miaka 13.

  Nimeokoka na Mume wangu ameokoka na anapenda sana kuwahubilia watu habar za wokovu. Hivi karibun aliniambia tunategemea mgeni kutoka Marekan. Mgeni huyo ni dada wa rafiki yake. Kwakwel alihakikisha chumba anachofikia kina kila kitu. Nilijitahid kufanya vile alivyokua anataka.
  Mgen alifika na yeye ndiye aliyeenda airport kumpokea. Alipofika nyumban nilimpokea kwa moyo mmoja na alikuja na binti yake wa miaka 7. Kilichokua kinaniuma zaidi Muda wa kumuhubilia walikua wanakaa kochi 1. Muda wa kula unapofika mume wangu ndo anamkaribisha chakula na wakat mwingine nakua sijamaliza kutenga.

  Wakat wa kula hukaa pamoja mezan yani kiti cha mume wangu,kinachofata cha huyo dada na kingine cha mtoto wake. Mimi najikuta nakaa mbali kabisa na mume wangu. Nilipomwambia akanijibu KWANI TATIZO LIKO WAPI? HUKO KAZINI HUWA UPO NA MIMI? Nikamwambia caring unayoionyyesha imezid. Hujawahi hata siku moja kunivutia kiti ili nikae iweje huyu unamjali hivyo? Akanambia nimekuelewa.

  Sasa huyu dada akaniaga anakwenda kusalimia kwa aunt yake. Aliondoka asubuh na mume wangu akasema anampeleka. Kiukwel ilipofika saa 12 jion nilimpigia simu mume wangu kutaka kujua yupo wapi mana si kawaida yake kuchelewa kurud. Alipopokea akanijibu kwa hasira nampeleka wifi yako kwa aunt yake. Nikamwambia mbona hata hujanambia km utampeleka jion na mmeondoka asubuh? Nikakata simu. Aliporud nikamwambia ulivyofnya sio vizur ulipaswa kunijulisha kilichokufanya uchelewe. Akanijibu nimekaa miaka mingi hakuna wa kuniuliza swali km hilo. Nikamwacha mana sikutaka marumbano.

  Sasa leo amesahau IPAD yake nikawa naangalia. Nikakuta kale katoto kamejirecord video na wapo eneo la ufukwen. Yupo mume wangu,huyo dada na huyo aunt yake wanakula huku wakipiga story.

  Naomba ushaur nifanyaje? Nisamehe na nisimuulize?

 2. Pole sana na unayokutana nayo. Hapo inabidi mkae wawili umuulize kwa utaratibu ili akueleze kwa kirefu nini kinaendelea. Wewe ni mke wake na unahaki ua kujua yupo wapi na anafanya nini, unahaki ya kuwa karibu naye wakati wote na haifai mtu mwingine aingilie kati yenu. Endelea kumuomba Mungu akufunulie kama kuna jambo lolote linaloendelea kati yao.

 3. Pole sana dada mpendwa, kumbuka kuwa huyo mume ulipewa na mungu na hakuna mtu anayeweza kuivunja ndoa yako. Najua unawakati mgumu kwa sasa lakini mungu alitupa roho ya upendo na uvumilivu , usikurupuke na ukaharibu kila kitu jambo la kufanya jipe moyo na umwombe mungu akupe ujasiri for the time been ili ukusanye ushahidi dhidi yao, ukiweza chukua hiyo video script na uisave sehemu fuatilia mienendo yao, subiri muda kidogo na umwambie mumeyo kuwa unamtoa out wakati mpo kwenye normal state anza kumuuliza taratibu na kama ana hofu ya mungu atakueleza wazi what is going on with that lady. kumbuka wewe ni nguzo ya familia na bibilia inasema mwanamke mpumbavu huivunja nyumba yake kwa mikono yake, simama imara kwa kuomba na mungu atakuonyesha njia pasipo na njia.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s