Fedha Katika Ndoa

Maswala ya fedha huleta changamoto nyingi kwenye ndoa. Wanandoa wengi hukwepa kulizungumzia suala hili. Tafiti zinaonyesha mojawapo ya sababu ya ndoa nyingi kuvunjika ni usiri na kutokuaminiana katika masuala ya fedha.

Wanandoa ni mwili mmoja, haipaswi kufichana jambo lolote. Inawapasa kukaa kwa pamoja mume na mke mkaangalia vyanzo vyenu vya mapato na mkapanga bajeti ya jinsi gani mtatumia fedha zenu kwa ustawi wa familia yenu. Uwazi katika mambo ya fedha ni muhimu sana, matumizi yote yajulikane na kila mmoja na pia matumizi makubwa yajadiliwe kwa pamoja kabla ya kufanya maamuzi.

Jambo lingine la muhimu ni kushirikishana pale unapotaka kumsaidia mtu. Usitoe msaada wa kifedha bila kumshirikisha mwenzi wako. Pale atakapokuja kuambiwa asante kwa kitu fulani wakati hana habari hatajisikia vizuri na atahisi kuna mengi mengine unamficha. Ndoa imara ina ushirikiano, kuaminiana na kuheshimiana katika mambo yote.

Advertisements

2 thoughts on “Fedha Katika Ndoa

 1. Shalom.

  Ndoa ni kuaminiana katika kila jambo. Si pesa peke yake vitu vingi tu vya kushirikishana au kushirikiana. Jambo kubwa si FEDHA peke.

  mm binafsi nadauti sana jambo hilo. Vitu vingi nimefanya na wala sikuona tofauti ya NDOA pesa na kushirikishana.

  mm nieokoka mwaka 2001 nikiwa KARISMATIKI na sasa niko kwa BABA yangu JOHN SAID UKONGA (UDHIHIRISHO WA INJILI) mwaka wa 3 sasa.

  Jambo kubwa ni kumtegemea mungu wako wa NDOA yako uliyenaye.

  Asemaye : Lucy K.

 2. Nashukuru sana kwa net hii na mafundisho yake. Kweli tunahitaji sana mafundisho ya ndoa wakati tulionao. Mi nina 7 yrs ktk ndoa ni vizuri sana kuaminiana wapenzi ktk pesa na kila kitu. Mimi na mme wangu tunaaminiana sana hata ktk issue za pesa. Pia kwa sababu tunaaminiana tuna uhuru fulani wa kutumia pesa hata bila kumwambia mwingine mladi isiwe pesa nyingi. Kabla ya kuoana kila mtu alikua na account yake na baada ya kuoana tukaamua tuendelee hivyo hivyo na tuna uhuru wa kutumia account zetu interchangeably. Mungu ametubariki sana sana wapendwa!!!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s