Amnon na Tamari: Tamaa ya Mwili na Sio Upendo

Somo: 2 SAM. 13:1-17

“Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda. Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya umbu lake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni vigumu kumtendea neno lo lote. Lakini Amnoni alikuwa na rafiki, jina lake Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi; naye Yonadabu alikuwa mtu mwerevu sana. Naye akamwambia, Kwa nini, Ee mwana wa mfalme, unakonda hivi siku kwa siku? Hutaki kuniambia? Amnoni akamwambia, Nampenda Tamari, umbu la ndugu yangu, Absalomu. Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile mkononi mwake. Basi Amnoni akalala, akajifanya mgonjwa; na mfalme alipokuja kumtazama, Amnoni akamwambia mfalme Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, aniandalie mikate miwili machoni pangu, nipate kula mkononi mwake. Basi Daudi akatuma mjumbe aende nyumbani kwa Tamari, akasema, Nenda sasa nyumbani kwa Amnoni, ndugu yako, ukamwandalie chakula. Akaenda Tamari nyumbani kwa nduguye Amnoni; naye alikuwa amelala. Akachukua unga, akaukanda, akaiandaa mikate machoni pake, akaioka mikate. Akalitwaa kaango, akaisongeza mbele yake; lakini alikataa kula. Naye Amnoni akasema, Toeni watu wote kwangu. Wakatoka kila mtu kwake. Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani. Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu. Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu. Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa. Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako. Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza. Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake.”

Habari hii inaonyesha jinsi Amnon alivyokuwa akimtamani dada yake wa kambo tamari kimwili na yeye kudhani kuwa anampenda. Alifikia hadi kuugua kutokana na tamaa yake, na badala ya kutafuta ushauri wa busara toka kwa baba yake Daudi au watumishi wa Mungu yeye akatafuta ushauri toka kwa rafikiye ambaye ni mwerevu wa kidunia na sio kwa misingi ya Mungu. Alipopewa ushauri aliufanyia kazi na akambaka ndugu yake tamari. Baada ya tendo hilo akagundua kuwa hampendi tamari na hajawahi kumpenda. Akamfukuza na kuita mjakazi wake amfukuze ‘mwanamke’ huyu. Baada ya kulala naye hakuwa tena binti mrembo tamari bali ‘mwanamke huyu.’
Somo hili tunajifunza mambo makuu yafuatayo:
1. Tamaa ya mwili ni tofauti na upendo, upendo hutafuta kumpendeza umpendaye kwa gharama yoyote bali tamaa hutafuta kuipendeza nafsi kwa gharama yoyote.

2. Tamaa haikupi muda wa kufikiria matokeo ya maamuzi utakayochukua kwako na kwa mtu umpendaye bali Upendo hufikiria matokeo kwanza kabla ya kufanya maamuzi.

3. Tamaa ikitimizwa hugeuka kuwa chuki bali upendo huzidi kuimarika pale unapomtendea wema yule unayempenda.

4. Upendo huvumilia bali tamaa haina uvumilivu kabisa.

Ubarikiwe unapojiepusha na wakina Amnon wa kisasi hiki maana wapo wengi, anaweza asitumie nguvu ya kukukamata bali akatumia nguvu ya maneno na ukisha kulala naye akakutupa na asikujue tena.

5 thoughts on “Amnon na Tamari: Tamaa ya Mwili na Sio Upendo

  1. Welcome. Just follow this blog and you will receive all notifications and announcements. Karibu sana

  2. Amina.nimejifunza pia tunapokuwa na sauti mbili zinazokinzana mioyoni mwetu ni vyema kumwomba ROHO MTAKATIFU atushauri tuamue vyema.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s