Maalumu kwa Wanaume Wote…

Leo nataka kuongea na wababa. Wanawake wengi wamekuwa stressed sana baada ya kujifungua na kujikuta wamebadilika maumbo yao hasa tumbo na kunenepa. Wanawake hawa hujitahidi kwakweli kufunga tumbo na njia nyingi ili kurudia hali ya kawaida. Miili haifanani, wengine hufikia hivyo mapema kuliko wengine, wengine huwa ni ngumu sana sana na wengine huamua kutonyonyesha kabisa ili wasile. Kumbuka tumbo la mama huyu limestrech slowly for nine months. Na mwili umeongezeka kidogo kidogo kwa muda mrefu, hivyo huwezi tarajia arudie hali yake overnight.

Tatizo ndio huanzia hapa. Utakuta mume anaanza kumsimanga mkewe “angalia ulivyojinenepea, tumbo baya limejaa michirizi, mbona fulani karudia hali yake, n.k n.k”, jamani miili haifanani, hilo tumbo unaloona limejaa michirizi ni sababu watoto wako uwapendao sana walitafuta hifadhi huko. Sisemi wanawake tusirudie hali za mwanzo, la, ila mume usimsimange mkeo sababu ya mabadiliko ya mwili sababu ya uzazi. Pamoja mtafute njia za kumsaidia, mnaweza ruka kamba pamoja, situps mkafanya pamoja na mazoezi mengine. Wengi wetu muda wa kwenda gym au kukimbia haupo, ila pamoja mnaweza kusaidiana.

Diet husaidia sana, ila diet sio kazi rahisi. Wewe mume unataka mke akupikie mapochopocho ila yeye aishie kula mboga na matunda, Inawezekana kweli??? Fanya naye diet kuonyesha ushirikiano. Kumsimanga sababu ya unene au ukubwa wa tumbo hakumsaidii zaidi kutampa stress ambazo zitamfanya azidi kula. Hivi ni wanaume wangapi wamewahi kufanya diet??? Diet sio lelemama, hivyo msupport na sio kumsimanga.  Tena ukiangalia hao wanaowasimanga wake zao wao ni wanene na wanavitambi ila wake zao hawawasimangi. Leo unamchukia sababu amenenepa, je umewahi waza itajuwaje akikatwa ziwa?? Na akipata fistula je?? Mtu kakuletea watoto wazuri kwa uchungu mkubwa na mara nyingine operation, kachungulia kaburi, shukrani yako inakuwa kumsimanga???

Advertisements

8 thoughts on “Maalumu kwa Wanaume Wote…

 1. Magreth asante kwa ujumbe mzito….ila hiyo excuse ya kusema kuwa miili sijui ipo tofauti si kweli ni kujiachia na kutafuta sababu…maana kama kabla ulikuwa na mwili wa kawaida ina maana unaweza kabisa kurudi kuwa kawaida au kuzidi japo kidogo na si kuwa tepetepe..unless kama una mwili huo mnene hata kabla ya uzazi..!

  ..me sijui ni chakula au uzembe au ??? maana wanawake wa nchi nyingine hasa za ulaya wakizaa wengi tu utawakuta wako na shape nzuri immediately baada ya uzazi…ila nachojua wanafanya mazoezi sana kabla, wakati wa mimba na baada ya kuzaa..na kila kitu cha ndani wanafanya wenyewe (kama ni single mother) au kwa kusaidiana kiasi na husband…but wanawake wa tz akiwa na mimba na kuzaa ataongeza housegals na kuwa nao wawili mpaka watatu..so mwendo utakuwa ni kula sana (sababu ya kunyonyesha??) lakini no mazoezi (kila kitu wanafanya mahousegals) na mwisho wa siku mwili unapoteza mwelekeo…hv kwann wadada ulaya (na hata vijijini tanzania) hawana mahousegal but wa tz-mjini mahousegal mpaka watatu?utasema ni sbbu ya kazi mjini..bt ulaya wanawake wanafanya kazi sana (bila likizo ndefu za uzazi) tena bila kuzuga (maana ni kulipwa kwa hrs na si attendance)kama wadada wa tz-mjini na wadada wa tz-vijijini ndio funga kazi kwa kuwork hard..!

  …nadhani hawasimangwi ni vile tu wanaambiwa ukweli na ukwel mara nyingi unauma…maana kama mtu unajaribu kumlipia hata gym lakini hataki kubadilika..ukitaka hizo kauli za ”kusimangwa” ziishe ni rahisi tu kwa kuamua kurudisha discipline ya mwili..!

  conrad

 2. Asante kwa kuleta mada hii. Samahani aliyeiandika ila naona haiko balanced na imeandikwa kwa jazba na kisasi na haiwezi kutusaidia sisi wanawake wakristo. Nakubaliana kiasi na mwandishi kwamba ni vema Me amsaidie Ke ili mwili urudi kuwa mzuri. Ni ukweli usiopingika Ke wengi wanajiachia sana hapa Tz hasa wadada wenye social status. Yaani akijifungua tu baaaaasi tena. Naheshimu sana akina Ke wote kwa mchango wao mwingi ktk familia lakini sikubaliani na hili la kujiachia hata kidogo. Kiafya sio nzuri na pia kwa Me wengi hawapendi wanawake wao kua nenez!!! binafsi mme wangu hapendi niwe mnene so niko cautious hata baada ya kujifungua i take care of myself. Nimesikia wanawake wengi wakisema waume zao hawapendi wawe wanene so trend ya waume ndo hiyo. Pia akina mama unafaa upendeze usiwe too slim au fat, Wanawake tubadilike !!!!!!!!!!!!

 3. Nashukuru kwa mchango wako, ila umekosea kusema nimeandika kwa jazba. Mimi ni mwandishi ninayejua nini cha kuandika na kwa faida ya nani chini ya uongozi wa Roho mtakatifu. Kama kwako kupungua sio tatizo mshukuru Mungu maana wenzio wanahangaika mchana na usiku. Weighloss struggle sio hapa Tanzania tu ni tatizo la dunia nzima, so badala ya kuwahukumu kuwa wanajiachia waeleze wafanye nini katika struggle hiyo.

  Hapa naongea na watu wa aina zote hivyo siwezi kutumia reference ya mtu mmoja, ni ukweli usiopingika kuwa dieting is very hard na inahitaji discipline ya hali ya juu hivyo support ni muhimu sana kuliko lawama, na criticms.

 4. jaman mada imenigusa sana,Tuambie tufanyaje il tuweze fanya diet,mie kila nikijaribu nashindwa, nakuwa na njaa sana.

 5. mi binafsi nashkuru kwa kuwaelimisha wanaume,kwani najua wanawake baada ya kujifungua wanaweza rudia hali yao ya awali but not 100parcent,huwez kuwa km ulivyokua msichana exactly,so ni muhimu kuwapa elimu hii wnaume,kubeba mtoto c jambo la mchezo mpk kuja kumleta duniani.mmh!ni kazi kweli.

 6. Mada ipo poa but kinacholeta mwili baada ya kujifungua ni msosi aisee acha kunywa mtori na miuji uone

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s