Mshukuru Mungu Kwa Wema Wake

ZAB. 95:2-3
“Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi.  Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu, Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.”

ZAB. 107:1
“Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.”

Tumekuwa na orodha ndefu za prayer points kila siku. Kila tunapoamka, mchana kutwa na tunapolala tumejaa maombi mengi kwa Mungu wetu. Mungu wetu amekuwa mwaminifu sana na hutujibu maombi na kututendea mengi mengine ambayo hata hatukuomba wala kutarajia. Lakini je ni mara ngapi umekwenda mbele za Mungu kwa nia ya kumshukuru tu kwa mengi anayokutendea, kwa uaminifu wake na kwa rehema zake?

Kuna nguvu kubwa katika kumshukuru Mungu. Kuna kutiwa moyo katika kuyatafakari yale mengi aliyokutendea na kumshukuru kwayo. Wale wakoma tisa walipopona hawakurudi kumshukuru Bwana Yesu, lakini mmoja wao alirudi miguuni kwa Yesu na kushukuru kwa uponyaji, Yesu alimwambia imani yake imemuokoa, hivyo zaidi ya uponyaji alipokea na wokovu.

Siku ya leo chukua kalamu na daftari, utafakari yote ambayo Mungu amekutendea na hakika roho yako itainuliwa, nafsi yako itaimarishwa na imani itaongezeka. Ukifanya maombi leo usiombe lolote bali mshukuru Mungu kwa hayo uliyoyaandika, hakika utaona jinsi utakavyojaa nguvu za Mungu na kutiwa moyo kuzidi kusonga mbele na yale unayoyaona ni magumu utayaona kuwa si kitu mbele za Mungu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s