Utii kwa Mume na Upendo kwa Mke

EFE. 5:22-29, 33

“Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.    Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.”

Wengi wetu tumeshaisikia mistari hii sana na yumkini hata kuikariri, lakini je ni wangapi wanaiishi? Mistari hii inaanza kuwaasa wake kuwatii waume zao kama kanisa linavyomtii kristo. Hili ni agizo kwa wake wote bila kujali mume anakutendea nini, anaelimu kiasi gani, anakipato kiasi gani, ameokoka au hajaokoka.  Kumtii mume ni kukubali kuwa chini ya uongozi wake, kumwamini anavyoongoza familia, kumstahi na kumheshimu.

Ukimuheshimu mume huwezi kufanya mambo na kumficha, huwezi kumsemesha vibaya mbele za watu, huwezi kufanya maamuzi bila kumshirikisha, utamhudumia katika hali zote kwa upendo bila kumkebehi.

Waume nao wanapaswa kuwapenda wake zao kama Kristo anavyolipenda kanisa, huu ni upendo mkuu sana. Kristo amelipenda kanisa bila kujali kanisa limemfanyia nini, upendo wa agape. Hata kama mkeo amekosea kiasi gani, upendo wako lazima uwe mkubwa kuliko kosa lake na uwe tayari kumrejeza kwa upendo, jambo hili sio dogo linahitaji neema ya Mungu.

Umpende mkeo kama mwili wako, ukimtunza na kumlisha. Kumpenda katika hali zote, ukimmpenda mke wako utamtunza, utamlinda, utamtia moyo, utahakikisha Ana furaha wakati wote na utajitoa nafsi yako kwa ajili yake bila kujihurumia.

Huu ndio msingi wa ndoa imara, tukifika hapa ndoa zetu zitakuwa zenye amani na furaha siku zote.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s