Mwanamke Atamlinda Mwanaume – Kwa Maombi!

YER. 31:22
“Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.”

Mwanamke atamlindaje mwanaume?
Je, kwa kupokea simu zake?
Je, kwa kwenda naye kila mahali?
Je, kwa kupekuwa simu, facebook na email zake?
Je, kwa kugombana na kila anayeongea naye?
Je, kwa kwenda kwa wagaga na kumzindika?
Je, kwa kumuwekea mobile tracking device?
Je, kwa kumuwekea wapelelezi wamfuatilie?

HAPANA! Neno la Mungu linasema Bwana asipoulinda mji yeye akeshaye afanya kazi bure. Mume au mchumba analindwa na Mungu, mkabidhi kwa Bwana kwenye maombi, mfunike na damu ya Yesu kila siku naye atakuwa salama. Hauna haja ya kila saa kupiga simu kumuuliza “upo wapi”, “upo na nani”, “nakuja hapo sasa hivi”, utapata magonjwa ya moyo bure. Mwanamke atamlinda mwanaume kwa kumuombea daima!

Usiku mwema, usilale wala kwenda mahali asubuhi bila kumlinda mume wako KWENYE MAOMBI!!!

Advertisements

6 thoughts on “Mwanamke Atamlinda Mwanaume – Kwa Maombi!

 1. Bwana Yesu asifiwe dada.
  Najiuliza sana nitawezaje kumwombea mume wangu wakat ananiumiza kwa majibu yake ya karaha?
  Mara nyingi napotaka kumwombea huwa nakumbuka majibu ya kukatisha tamaa. Mara nyingi ananiambia mimi nipo kimwili yani mtu wa nafsi.
  Mfano leo asubuh kunawagen walikuja. Nikamuuliza ” unaapointment na mtu yeyote? Akanijibu maswali ya nn wewe tuma mtu akafungue geti. Unauliza sahiz kwan usiku? Kwakwel niliumia nikabak nalia tu. Visa ni vingi na ameokoka.
  Nisaidie nifanyaje ktk hali km hz zinapontokea.
  Asante na ubarikiwe.

 2. Majaribu hayan budi kuja cha mcngi ni kuomba bila kukata tamaa,na kuwa na moyo wa msamaha.

 3. Amina dada Suzan nimekupata. From today ntazid kumpenda na kumtii mume wangu no matter what he did to me. Mungu akubariki.

 4. Bwana Yesu asifiwe wapendwa! Mstari huu wa Jeremiah una maana gani hasa? naombe mnifafanulie zaidi kwa msaada wa Roho Mtakatifu. kwani kuna mahala wamefananisha kuwa maana yake ni Kanisa litamzungukia Bwana, ikimaanisha Mwanamke ni Kanisa na Mwanaume imetumika kumaanisha MUNGU. Mbarikiwe!

 5. Hakuna lisiliwezekana kwa Mungu.unaposema nimechoka yy ndo anaanzia hapo kikubwa ni kuwaombea tu waume zetu tukiwa na moyo wa upendo msamaha, shukran na uvumilivu.tukifanya hivo tutashinda, tusichoke kuwaombea jaman.akikujibu vibaya mwambie baba samahan na baaada ya hapo ingia chumban omba msamaha kwaajili yako na yake.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s